title : TAIFA STARS YAKWEPA FITINA UGANDA
kiungo : TAIFA STARS YAKWEPA FITINA UGANDA
TAIFA STARS YAKWEPA FITINA UGANDA
Wakati kesho Jumamosi Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, ikitarajiwa kucheza mechi ya kufuzu kwa Fainali za Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) dhidi ya Uganda, kikosi hicho jana Alhamisi kilikwepa kiunzi kimoja cha wenyeji wao, Uganda.
Taifa Stars ambayo imepangwa Kundi L katika michezo hiyo ya kufuzu Afcon, kesho Jumamosi itacheza na Uganda katika Uwanja wa Mandela uliopo Kampala, Uganda.
Kiunzi ambacho Taifa Stars imekiruka ni cha kukwepa hujuma za wenyeji wao hao baada ya kupanda basi lingine tofauti na lile waliloandaliwa na Shirikisho la Soka la Uganda (Fufa).
Championi ambalo lilikuwepo wakati Taifa Stars inawasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebe majira ya saa 10:40 jioni, lilishuhudia kikosi hicho kikipanda basi ambalo wamekuwa wakilitumia siku zote wanapokuwa Tanzania.
Basi hilo lilisafi ri kutoka jijini Dar es Salaam mpaka Uganda likiwa na mashabiki wa timu hiyo ambao wameamua kutua hapa Uganda kutoa sapoti kwa Taifa Stars.
Taarifa zinaeleza kuwa Fufa waliandaa basi ambalo lingeuchukua msafara wa Taifa Stars, lakini mashabiki wa timu hiyo wakaamua kupeleka basi lao ilikama kulikuwa na hujuma zozote za wenyeji wao, wazikwepe.
Muda mfupi baada ya kikosi hicho kutua, kocha mkuu, Emmanuel Amunike alisema: “Tunashukuru kwa kufi ka salama hapa Uganda, wachezaji wanaonyesha morali ya hali ya juu ambapo matumaini yanaonyesha kwamba tutaibuka na ushindi.
Hivyo makala TAIFA STARS YAKWEPA FITINA UGANDA
yaani makala yote TAIFA STARS YAKWEPA FITINA UGANDA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TAIFA STARS YAKWEPA FITINA UGANDA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/taifa-stars-yakwepa-fitina-uganda.html
0 Response to "TAIFA STARS YAKWEPA FITINA UGANDA"
Post a Comment