title : KAMBI YA TIMU YA YAIFA YA SOKA LA UFUKWENI KUVUNJWA JUMAPILI
kiungo : KAMBI YA TIMU YA YAIFA YA SOKA LA UFUKWENI KUVUNJWA JUMAPILI
KAMBI YA TIMU YA YAIFA YA SOKA LA UFUKWENI KUVUNJWA JUMAPILI
kIkosi cha timu ya Taifa ya soka la Ufukweni wakiwa katika picha ya pamoja.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya soka ya ufukweni (Beach Soccer) Boniface Pawasa amesema kuwa kwa sasa anavunja kambi rasmi siku ya Jumapili kwa ajili ya wachezaji kurudi nyumbani baada ya wapinzani wao Afrika Kusini kujiondoa kwenye mechi ya kuwania nafasi ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON Nchini Misri.
Akizungumza leo, Pasawa amesema kuwa kambi waliyokuwa wameweka na wakiendelea na mazoezi kwenye Fukwe za Coco Beach ilikua ni kwa ajili ya kujiandaa na mchezo ho na Afrika Kusini ambapo wamejitoa tayari.
"Lengo letu la kwanza ilikuwa ni mechi dhidi ya Afrika Kusini lakini wamejitoa tayari ambao ulikua ni mchezo wa kufuzu kwenda Mataifa Afrika (AFCON) na tutawalipa wachezaji wote stahiki zao ili warejee majumbanu," amesema Pawasa.
Amesema, katika maandalizi yajayo kwa ajili ya michuano ya kuwa wameshatuma maombi kwa timu ya Taifa ya Oman kwa Kocha Talib Hilal kwa ajili ya kuweza kupata kambi ya wiki mbili kabla ya kwenda nchini Misri kuchuana katika michuano hiyo ya AFCON.
"Wenzetu Oman ni wazoefu wameweza kucheza hata mashindano ya dunia kwahiyo kupata nafas ya wiki mbili nchini mwao itakuwa ni nafasi nzuri sana kwetu kwa maandalizi ya AFCON, ukiangalia Oman na Misri sio mbali,"amesema.
Pawasa amesema kuwa mpaka sasa ameshaomba mechi za kirafiki kwa timu ya Malawi na Uganda kwa ajili ya kupata mchezo wa kirafiki kujiandaa na michuano ya AFCON miezi mitatu ijayo.
micAmeeleza kuwa mbali na hilo atakuwa na programu ya kuweza kuwapata wachezaji wengi wa mchezo huo mwezi Oktoba mwaka huu na kuwataka wachezaji wa mpira wa miguu kuja kutafuta fursa baada ya kushindwa kuoata nafasi kwenye timu ya taifa ya mpira wa miguu.
Mbali na hilo, Pawasa amewaomba watanzania waweze kujitokeza kuisaidia timu ya taifa ya soka la ufukweni kwani ni timu inayowakilisha nchi na sio klabu, wasiwaachie majukumu yote Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) kwani imechukua miaka takribani 30 kuweza kufuzu kwenda Michuano ya AFCON na malengo yakiwa ni kuhakisha wanapata nafasi ya kwenda Kombe la Dunia nchini Paraguay.
Timu ya Taifa ya Soka la Ufukweni ya Tanzania imefuzu kucheza Fainali za Africa zitakazofanyika nchini Misri.
baada ya mpinzani wake Afrika Kusini kuwasilisha barua ya kujiondoa katika mashindano.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) tayari wametuma barua hiyo ya kufuzu kucheza Fainali hizo za Afrika zitakaofanyika Misri mwaka huu kuanzia Desemba 9-Desemba 14,2018 na kushirikisha nchi Nane.
Timu ya Soka la Ufukweni ilikuwa kambini kujiandaa na mchezo huo uliokuwa uchezwe Jumapili Septemba 9,2018 na kambi hiyo itavunjwa rasmi Jumapili.
Hivyo makala KAMBI YA TIMU YA YAIFA YA SOKA LA UFUKWENI KUVUNJWA JUMAPILI
yaani makala yote KAMBI YA TIMU YA YAIFA YA SOKA LA UFUKWENI KUVUNJWA JUMAPILI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KAMBI YA TIMU YA YAIFA YA SOKA LA UFUKWENI KUVUNJWA JUMAPILI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/kambi-ya-timu-ya-yaifa-ya-soka-la.html
0 Response to "KAMBI YA TIMU YA YAIFA YA SOKA LA UFUKWENI KUVUNJWA JUMAPILI"
Post a Comment