RC NDIKILO -AUNDA TUME NDOGO KUFUATILIA SAKATA LA MWENYEKITI WA DUTUMI KUKATALIWA

RC NDIKILO -AUNDA TUME NDOGO KUFUATILIA SAKATA LA MWENYEKITI WA DUTUMI KUKATALIWA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa RC NDIKILO -AUNDA TUME NDOGO KUFUATILIA SAKATA LA MWENYEKITI WA DUTUMI KUKATALIWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : RC NDIKILO -AUNDA TUME NDOGO KUFUATILIA SAKATA LA MWENYEKITI WA DUTUMI KUKATALIWA
kiungo : RC NDIKILO -AUNDA TUME NDOGO KUFUATILIA SAKATA LA MWENYEKITI WA DUTUMI KUKATALIWA

soma pia


RC NDIKILO -AUNDA TUME NDOGO KUFUATILIA SAKATA LA MWENYEKITI WA DUTUMI KUKATALIWA

NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 
MKUU wa Mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ameunda tume ndogo kufuatilia malalamiko ya baadhi ya wajumbe wa serikali ya kijiji cha Dutumi ,Kibaha, kumtaka mwenyekiti wao Mkali Kanusu ajiuzulu kwa kukiuka taratibu za uongozi.

Mwenyekiti huyo anadaiwa kufanya ubadhirifu wa fedha,kuuza maeneo ya kijiji,kugawa ardhi bila ya utaratibu,vitabu tisa kuibiwa,kugomea mkutano na kutosoma mapato na matumizi.

Ndikilo,  alifikia maamuzi hayo baada ya kusikiliza pande zote mbili za mwenyekiti na wajumbe wa kijiji ambao walimpinga  kwenye kikao cha ndani na kikao cha nje cha wananchi.

"Tume hii itaenda kufanya kazi kwa muda wa wiki moja kisha itatupa majibu kama ajiuzulu ama aendelee na nafasi yake ili shughuli za maendeleo ziendelee ".

"Shughuli za maendeleo zimesimama kwa muda mrefu sasa ambapo barua za malalamiko zimefika hadi kwa Rais hivyo lazima suala hili lifikie mwisho," alisema Ndikilo.

Alisema baada ya barua ya walalamikaji iliandikwa kwa mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kibaha ambaye alimwambia mtendaji amwandikie mwenyekiti ili ajibu tuhuma zinazomkabili ndani ya siku tisa kuanzia tarehe 19 hadi 29 awe amejibu.

"Hata hivyo hakujibu lakini vyombo mbalimbali vilianza kufuatilia suala hilo ambao ni Takukuru,ofisa utumishi,kamati ya ulinzi na usalama na mkaguzi wa ndani hata hivyo hakukubali wala kukanusha," alisema Ndikilo.

Mwenyekiti huyo ambae pia ni diwani wa Dutumi,  Mkali Kanusu alisema , tuhuma zote anazopewa hazina ukweli.

Kwa upande wake, mkuu wa wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama alielezea suala hilo linaenda kisiasa kwani hata watu waliomkubali walikuwa wengi.
 MKUU wa Mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,akizungumza huko kijiji cha Dutumi ,Kibaha.(
Baadhi ya wananchi Dutumi, Kibaha Vijijini, wakimsikiliza, mkuu wa Mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo.
(Picha na Mwamvua Mwinyi).


Hivyo makala RC NDIKILO -AUNDA TUME NDOGO KUFUATILIA SAKATA LA MWENYEKITI WA DUTUMI KUKATALIWA

yaani makala yote RC NDIKILO -AUNDA TUME NDOGO KUFUATILIA SAKATA LA MWENYEKITI WA DUTUMI KUKATALIWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala RC NDIKILO -AUNDA TUME NDOGO KUFUATILIA SAKATA LA MWENYEKITI WA DUTUMI KUKATALIWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/rc-ndikilo-aunda-tume-ndogo-kufuatilia.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "RC NDIKILO -AUNDA TUME NDOGO KUFUATILIA SAKATA LA MWENYEKITI WA DUTUMI KUKATALIWA"

Post a Comment