Programu ya Vodacom Tanzania ya mafunzo kwa wahitimu vyuo vikuu kufanikisha kupata viongozi wa baadaye

Programu ya Vodacom Tanzania ya mafunzo kwa wahitimu vyuo vikuu kufanikisha kupata viongozi wa baadaye - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Programu ya Vodacom Tanzania ya mafunzo kwa wahitimu vyuo vikuu kufanikisha kupata viongozi wa baadaye, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Programu ya Vodacom Tanzania ya mafunzo kwa wahitimu vyuo vikuu kufanikisha kupata viongozi wa baadaye
kiungo : Programu ya Vodacom Tanzania ya mafunzo kwa wahitimu vyuo vikuu kufanikisha kupata viongozi wa baadaye

soma pia


Programu ya Vodacom Tanzania ya mafunzo kwa wahitimu vyuo vikuu kufanikisha kupata viongozi wa baadaye

Programu nyingi za mafunzo kwa wahitimu wa vyuo vikuu wasio na uzoefu wa kazi duniani kote, zimekuwa zinalenga kuwawezesha wasomi wenye utaalamu katika fani mbalimbali kuwa na dhamira ya kuajiriwa kwenye makampuni mbalimbali yanayohitaji wataalamu. Huwawezesha wahitimu hao kupata msingi na ujuzi kuhusiana na taaluma zao, sambamba na kuwaanda kuwa viongozi wa siku za mbele. 

Tofauti na programu nyingine za kuwafundisha wahitimu wa vyuo vikuu kazi,Programu ya Vodacom Tanzania (ambayo imeasisiwa na Vodafone Group) inajulikana kama ‘Gundua Vipaji vya Wahitimu wa Vyuo Vikuu). Humuwezesha mhitimu kufanya kazi kwenye vitengo muhimu vya kampuni.

Programu hii ya miaka 2 inalenga kuwapata viongozi wa baadaye wa kuendesha biashara za kampuni kutoka kwa wahitimu wa vyuo vikuu waliobobea katika fani mbalimbali.Kwa kushirikiana na vyuo vikuu vya hapa nchini,lengo ni kukuza vipaji na kuwapata wataalamu ambao watafanikisha kuiwezesha Vodacom kwenda sambamba na mabadiliko katika sekta ya mawasiliano. 

Programu hii ya ‘Gundua vipaji vya wahitimu wa Vyuo vikuu’ nchini Tanzania, ilizinduliwa rasmi mnamo mwezi Julai,mwaka 2015 na ilianza kwa kupokea maombi ya wahitimu 10 kutoka vyuo mbalimbali ambao walichukuliwa katika awamu ya kwanza ilipoanzishwa. 

Ili kujiunga nayo,mhitimu anapitia mchakato mkali uliowekwa, kuhakikisha wanapatikana washiriki wenye sifa zinazostahili. Wahitimu wanafanyiwa tathmini kwa njia ya mtandao,kupitia uelewa wa majukumu watakayotekeleza,tathmini kwa njia ya makundi,uwezo wa kuwasilisha mada na kujieleza na mahojiano ya uso kwa uso.
Wahitimu wa programu ya kampuni ya Vodacom Tanzania wakikata keki kusherehekea kumaliza programu ya miaka miwili iitwayo 'Discover Graduate'. Programu hii iliyoanzishwa July mwaka 2017 inalenga kufunza na kusaidia wanafunzi bora kutoka vyuo mbalimbali nchini kuja kuwa viongozi bora wa kesho.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Perece Kirigiti akimkabidhi Gervas Mfubusa, moja kati ya watahitimu waliochaguliwa kuingia kwenye programu ya 'Discover Graduate'. Discover Graduates ni programu ya miaka miwili iliyodhamiriwa kufunza na kusaidia wahitimu bora kutoka vyou mbalimbali nchini kuja kuwa viongozi bora wa kesho. 



Hivyo makala Programu ya Vodacom Tanzania ya mafunzo kwa wahitimu vyuo vikuu kufanikisha kupata viongozi wa baadaye

yaani makala yote Programu ya Vodacom Tanzania ya mafunzo kwa wahitimu vyuo vikuu kufanikisha kupata viongozi wa baadaye Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Programu ya Vodacom Tanzania ya mafunzo kwa wahitimu vyuo vikuu kufanikisha kupata viongozi wa baadaye mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/programu-ya-vodacom-tanzania-ya-mafunzo.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Programu ya Vodacom Tanzania ya mafunzo kwa wahitimu vyuo vikuu kufanikisha kupata viongozi wa baadaye"

Post a Comment