RAIS MAGUFULI KUANZA ZIARA MKOANI SIMIYU KESHO SEPTEMBA 08

RAIS MAGUFULI KUANZA ZIARA MKOANI SIMIYU KESHO SEPTEMBA 08 - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa RAIS MAGUFULI KUANZA ZIARA MKOANI SIMIYU KESHO SEPTEMBA 08, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : RAIS MAGUFULI KUANZA ZIARA MKOANI SIMIYU KESHO SEPTEMBA 08
kiungo : RAIS MAGUFULI KUANZA ZIARA MKOANI SIMIYU KESHO SEPTEMBA 08

soma pia


RAIS MAGUFULI KUANZA ZIARA MKOANI SIMIYU KESHO SEPTEMBA 08

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake leo, kuhusu ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, ambaye anatarajia kuanza ziara ya siku tatu(03) kuanzia Septemba 08 hadi Septemba 10, 2018.

Na Stella Kalinga, Simiyu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli atafanya ziara ya siku tatu (03) Mkoani Simiyu, kuanzia kesho tarehe 08/09/2018 hadi tarehe 10/09/2018, Mkoani Simiyu.

Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake Mkuu wa Mkoa Mhe. Anthony Mtaka amesema Mhe. Rais akiwa mkoani Simiyu atapata nafasi ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo, kuweka mawe ya msingi, kufungua pamoja na kuzungumza na Wananchi kupitia mikutano ya hadhara.

Mtaka amesema siku ya Jumamosi tarehe 08/09/2018, Mhe. Rais atakagua na kuweka jiwe la msingi Ujenzi wa Mradi wa Maji wa Lamadi uliopo wilayani Busega na baadaye, ataelekea wilayani Bariadi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo(kushoto) na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Simiyu wakifuatilia mkutano kati ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Waandishi wa Habari, kuhusu ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, ambaye anatarajia kuanza ziara ya siku tatu(03) kuanzia Septemba 08 hadi Septemba 10, 2018.

Aidha, amesema Mhe. Rais akiwa katika Wilaya ya Bariadi, atafungua Jengo la Wagonjwa wa Nje(OPD) Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, atakagua na kufungua barabara za lami (kilomita 6.9) zilizojengwa chini ya mradi wa kuboresha Miundombinu ya Miji (ULGSP).

“Siku hiyo pia atakagua maendeleo ya Ujenzi wa  barabara ya Bariadi-Maswa inayojengwa kwa kiwango cha lami na kuweka jiwe la msingi. Mhe.Rais atapokea salamu za Chama Cha Mapinduzi, salamu za Wilaya, Mkoa, taarifa ya mradi wa ujenzi wa barabara na baadaye kuzungumza na Wananchi wa Mkoa wa Simiyu na Watanzania wote kwa ujumla, katika Mtaa wa Salunda kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Salunda.”
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ofisini kwake alipozungumza nao leo, kuhusu ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, ambaye anatarajia kuanza ziara ya siku tatu(03) kuanzia Septemba 08 hadi Septemba 10,2018.

“Tarehe 09/09/2018 Mhe. Rais atazungumza na wananchi wa wilaya ya Itilima eneo la Makao Makuu ya Wilaya (Lagangabilili) na kuelekea wilayani Meatu. Akiwa njiani kuelekea Meatu Mhe. Rais atapata fursa ya kusalimia wananchi wa Kijiji cha Mwandoya na baadaye atafungua Miundombinu ya Uboreshaji wa Huduma za Afya Hospitali ya Wilaya ya Meatu na kuzungumza na wananchi katika Viwanja vya Stendi ya Mwanhuzi” alisema Mtaka.

Ameongeza kuwa Siku ya Jumatatu tarehe 10/09/2018 Mhe. Rais Magufuli atahitimisha ziara yake Mkoani Simiyu kwa kuweka jiwe la msingi ujenzi wa daraja la Mto Sibiti linalounganisha Mkoa wa Simiyu na Singida na baadaye  kuwasalimia wananchi.

Katika hatua nyingine Mtaka ametoa wito kwa wananchi wote mkoani Simiyu hususani katika Miji ya Lamadi, Bariadi, Lagangabilili, Mwanhuzi na vitongoji vyake kujitokeza kwa wingi katika maeneo yote ambayo Mhe. Rais Magufuli atapita na kufanya mikutano ya hadhara.


Hivyo makala RAIS MAGUFULI KUANZA ZIARA MKOANI SIMIYU KESHO SEPTEMBA 08

yaani makala yote RAIS MAGUFULI KUANZA ZIARA MKOANI SIMIYU KESHO SEPTEMBA 08 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala RAIS MAGUFULI KUANZA ZIARA MKOANI SIMIYU KESHO SEPTEMBA 08 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/rais-magufuli-kuanza-ziara-mkoani.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "RAIS MAGUFULI KUANZA ZIARA MKOANI SIMIYU KESHO SEPTEMBA 08"

Post a Comment