title : NFRA YASISITIZA HAITONUNUA MAHINDI YASIYOKUWA NA UBORA
kiungo : NFRA YASISITIZA HAITONUNUA MAHINDI YASIYOKUWA NA UBORA
NFRA YASISITIZA HAITONUNUA MAHINDI YASIYOKUWA NA UBORA
Na Mathias Canal, NFRA-Dodoma
IKIWA msimu wa kununua mazao
umeanza, Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula
(NFRA), Vumilia Zikankuba amewataka wakulima kuhakikisha wanazingatia
ubora wa mahindi.
Aidha, amesema nchi inachakula
cha kutosha na kusisitiza kuwa katika msimu wa kwanza wa ununuzi wa mahindi bei
ya NFRA ni wastani wa Sh 380 hadi Sh 400 kwa kilo.Akizungumza na waandishi wa
habari ofisini kwake Mjini Dodoma, Zikankuba alisema NFRA haitaweza kununua
mahindi mabovu na kusisitiza wakulima kuwa na mahindi yenye ubora ambayo
yatawasaidia kupata masoko ya nje pia.
" Haiwezekani NFRA itumia
fedha za Serikali kununua mahindi yasiyokidhi viwango vya ubora na machafu
kutoka kwa wakulima. Hivyo wakulima wanapaswa kuzalisha mahindi kwa kuzingatia
viwango vya ubora vinavyokidhi vigezo vya soko..
Aliongeza: “Lazima chakula
tunachonunua kizingatie ubora. Tunataka tubadilishe taswira ya NFRA kwa sababu
awali kulikuwa na tatizo la chakula kuharibika kwa kipindi kifupi.”
Zikankuba alisema ili
kuhakikisha mahindi ya wakulima yanaweza kukidhi viwango vinavyotakiwa NFRA
tayari imekwishatoa elimu kwa wakulima kupitia vikundi na kwenye vyombo vya
habari.Alibainisha kuwa baada ya elimu
hiyo wakala umefanikiwa ambapo wakulima kutoka maeneo ya Makambako, Sumbawanga na
Mpanda wameanza kuzalisha na kuuza mahindi yenye ubora kwa NFRA.
“Changamoto iliyopo ni kwa
baadhi ya wakulima wachache ambao bado wamekuwa wagumu kubadilika na wale ambao
wanaamini wakitumia nafasi zao wanaweza kuuza mahindi yasiyo na ubora,"Alisema kwa mkulima kuwa na
mahindi yenye ubora unatoakiwa utasaidia katika kupata soko la NFRA, pia katika
taasisi zingine zinazonunua nafaka hiyo za ndani na nje ya nchi.
Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Vumilia Zikankuba.
Hivyo makala NFRA YASISITIZA HAITONUNUA MAHINDI YASIYOKUWA NA UBORA
yaani makala yote NFRA YASISITIZA HAITONUNUA MAHINDI YASIYOKUWA NA UBORA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NFRA YASISITIZA HAITONUNUA MAHINDI YASIYOKUWA NA UBORA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/nfra-yasisitiza-haitonunua-mahindi_84.html
0 Response to "NFRA YASISITIZA HAITONUNUA MAHINDI YASIYOKUWA NA UBORA"
Post a Comment