title : MKURUGENZI MKUU WA NSSF AFANYA MAZUNGUMZO NA TAASISI TATU ZA KIBENKI NCHINI
kiungo : MKURUGENZI MKUU WA NSSF AFANYA MAZUNGUMZO NA TAASISI TATU ZA KIBENKI NCHINI
MKURUGENZI MKUU WA NSSF AFANYA MAZUNGUMZO NA TAASISI TATU ZA KIBENKI NCHINI
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa ya Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bwana William Erio amefanya mazungumzo na Menejimenti ya baadhi ya Taasisi tatu za Kibenki hapa nchini ambazo ni NMB,CRDB na UBA kwa lengo la kuendeleza na kukuza mahusiano ya kibiashara.
Katika mkutano huo wameweza kuzungumza masuala mbali mbali yanayolenga kuimarisha ushirikiano utakaowezesha kukuza maendeleo katika sekta ya uchumi kupitia Benki zao na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF.
Wakurugenzi wakuu hao ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Bwana Charles Kimei,Bwana Usman Imam Isiaka Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya UBA pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB Ineke Bussemaker.
Wa kwanza pichani kulia Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ,Bwana William Erio akiwa kwenye mazungumzo na Menejimenti ya Benki ya CRDB ofisini kwake makao makuu jijini DSM ambapo wameweza kuzungumza masuala mbali mbali ya kuimairisha mahusiano baina yao.
Viongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na viongozi wa Benki ya CRDB wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao kwenye makao makuu ya NSSF ,katikati Mkurugenzi mkuu wa NSSF Bwana William Erio na pembeni yake ni mkurugenzi mkuu wa CRDB Charles Kimei na pembeni ni viongozi mbalimbali wa CRDB na NSSF.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya UBA ,Bwana Usman Imam Isiaka akielezea jambo wakati wa mazungmzo yake na Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bwana William Erio leo katika makao makuu ya NSSF jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya NMB Bi.Ineke Bussemaker akipongezana na Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bwana William Erio (Kulia) mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo baina yao ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Bwana Miichael Mungure amabaye ni MKuu wa kitengo cha akaunti na malipo(NMB), wa kwanza kulia ni Richard Mtapa ambaye ni Meneja Mwandamizi wa Taasisi za Serikali(NMB)
Hivyo makala MKURUGENZI MKUU WA NSSF AFANYA MAZUNGUMZO NA TAASISI TATU ZA KIBENKI NCHINI
yaani makala yote MKURUGENZI MKUU WA NSSF AFANYA MAZUNGUMZO NA TAASISI TATU ZA KIBENKI NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MKURUGENZI MKUU WA NSSF AFANYA MAZUNGUMZO NA TAASISI TATU ZA KIBENKI NCHINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/mkurugenzi-mkuu-wa-nssf-afanya.html
0 Response to "MKURUGENZI MKUU WA NSSF AFANYA MAZUNGUMZO NA TAASISI TATU ZA KIBENKI NCHINI"
Post a Comment