MFALME WA UINGEREZA KUKUTANA NA JPM.

MFALME WA UINGEREZA KUKUTANA NA JPM. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MFALME WA UINGEREZA KUKUTANA NA JPM., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MFALME WA UINGEREZA KUKUTANA NA JPM.
kiungo : MFALME WA UINGEREZA KUKUTANA NA JPM.

soma pia


MFALME WA UINGEREZA KUKUTANA NA JPM.

Mwanamfalme William wa Uingereza anapangiwa kukutana na rais wa Tanzania Dkt John Magufuli wiki ijayo wakati wa ziara yake ya siku saba Afrika.

Anatarajiwa kuzuru pia Kenya na Namibia katika ziara hiyo ambayo si ya kikazi.

Ziara hiyo itafanyika kuanzia 24 Septemba hadi 30 Septemba.

Lengo kuu la mwanamfalme huyo litakuwa kufuatilia juhudi za kukabiliana na ujangili na uhifadhi wa wanyama.

Atafanya ziara hiyo katika wadhifa wake kama rais wa mashirika yanayotetea uhifadhi wa wanyama ya United for Wildlife na Tusk Trust.

Amekuwa pia mlezi wa shirika la Royal African Society linalolenga kukuza uhusiano kati ya Afrika na Uingereza na hushiriki sana juhudi za kukabiliana na ujangili.

Akiwa ziarani Tanzania, Mtawala huyo wa Cambridge, atafanya mashauriano na Rais Magufuli kuhusu juhudi zinazopigwa na taifa hilo katika kukabiliana na ujangili na ulanguzi wa wanyama pori kwa mujibu wa shirika la habari la Press Association.

Kadhalika, atazuru bandari ya Dar es Salaam kujifahamisha zaidi kuhusu juhudi zinazopigwa na taifa hilo.

Tanzania imekuwa ikifanya juhudi kukabiliana na ujangili na ulanguzi wa wanyama.

Mwaka 2013, mwezi Oktoba, ilizindua Operation Tokomeza Ujangili ingawa ilisitishwa takriban mwezi mmoja baadaye, huku watetezi wa haki wakiwalaumu waliokuwa wanaendesha operesheni hiyo kwa ukiukaji wa haki za kibinadamu.

Tanzania ilikuwa na tembo 110,000 mwaka 2009 lakini idadi hiyo imeporomoka hadi kufikia tembo 43,000 kutokana na ujangili.

Moja ya malengo ya ziara ya Mwanamfalme William Afrika ni kupigia debe mkutano mkuu wa kukabiliana na ulanguzi wa wanyamapori ambao utaandaliwa jijini London kati ya 11-12 Oktoba.

Mkutano huo ambao kwa kirefu unafahamika kama Illegal Wildlife Trade Conference, unalenga kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kukabiliana na ulanguzi wa wanyamapori, kwa kuangazia mambo matatu makuu: ulanguzi wa wanyama, wadudu na mimea kama uhalifu, kujenga ushirikiano na kufunga masoko yanayotumiwa na wahalifu kulangua wanyamapori.

Taarifa ya Kensington Palace inasema ingawa atakuwa katika ziara ya kibinafsi, ameombwa na Malkia kutekeleza shughuli kadha rasmi kwa niaba yake.

Akiwa nchini Kenya, Mwanamfalme William atatembelea kikosi cha wanajeshi wa Uingereza cha 1st Battalion cha Irish Guards Battlegroup.

William huwa na cheo cha kanali wa jeshi la Ireland, na anatarajiwa kujifahamisha ni jinsi gani wanajeshi wa Uingereza na Kenya wanafanya kazi kwa pamoja kuimarisha shughuli zao.

Kikosi hicho cha Irish Guards Battlegroup hujumuisha wanajeshi wa Ireland na kundi la wanajeshi wa kenya ambao wamekuwa wakipokea mafunzo kutoka kwa kikosi cha jeshi la Uingereza.

Mwanamfalme William ameeleza wazi upendo wake kwa bara Afrika.

Aliomba posa kutoka kwa mkewe Kate Middleton wakiwa katika mgahawa mmoja wa porini karibu na Mlima Kenya mwaka 2010.

Mwanamfalme William, 36, majuzi alipokuwa anakubali kuwa mlezi wa shirika la Royal African Society alieleza anavyolipenda bara hilo.

"Nilianza kuipenda Afrika mara ya kwanza nilipokaa kwa muda Kenya, Botswana na Tanzania nikiwa bado kijana mdogo. Nilifurahia sana na nimekuwa nikitaka kurudi mara kwa mara kadiri iwezekanavyo tangu wakati huo," alisema.

Mara ya mwisho kwake kuzuru Kenya ilikuwa mwaka 2016 ambapo alikutana na Rais Uhuru Kenyatta na kushauriana kuhusu usalama na uhifadhi wa wanyama.

Wengi watasubiri kuona iwapo atasafiri na Catherine, Bintimfalme wa Cambridge.

Amekuwa katika likizo ya uzazi tangu mwezi Machi alipojifungua mwanamfalme Louis.

Lakini anatarajiwa kurejelea majukumu yake rasmi karibuni.

Wamejaliwa watoto wengine wawili, Mwanamfalme George, 5 na Bintimfalme Charlotte, 3.

Mwanamfalme William ni wa pili katika orodha ya warithi wa kiti cha ufalme wa Uingereza baada ya babake Mwanamfalme Charles, Mtawala wa Wales. chanzo Bbcswahili.














Hivyo makala MFALME WA UINGEREZA KUKUTANA NA JPM.

yaani makala yote MFALME WA UINGEREZA KUKUTANA NA JPM. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MFALME WA UINGEREZA KUKUTANA NA JPM. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/mfalme-wa-uingereza-kukutana-na-jpm.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MFALME WA UINGEREZA KUKUTANA NA JPM."

Post a Comment