title : MDAHALO WA WAZI WAKUPINGA UDHALILISHAJI WA WANAWAKE NA WATOTO.
kiungo : MDAHALO WA WAZI WAKUPINGA UDHALILISHAJI WA WANAWAKE NA WATOTO.
MDAHALO WA WAZI WAKUPINGA UDHALILISHAJI WA WANAWAKE NA WATOTO.
Khadija Khamis –Maelezo
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe, Riziki Pembe Juma aliwataka wazazi na walezi kutoa ushirikiano na Serikali kuhakikisha vitendo vya uzalilishaji vinaondoka nchini .
Hayo alisema leo huko katika kiwanja cha kufurahishia watoto kariakoo wakati wa mdahalo wa wazi wa kupokea maoni ya wananchi dhidi ya mapambano ya ukatili na udhalilishaji wanawake na watoto ulioandaliwa na Wizara ya Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto..
Alisema serikali imetunga sheria kwa wale wote wanaofanya vitendo vya udhalilishaji wanawake na watoto lakini kila siku vitendo vinaendelea hivyo iko haja ya mashirikiano ya pamoja kati ya walezi wazazi na serikali ili kuvidhibiti vitendo hivyo .
Aidha alisema tupange mikakati madhubuti kwa pamoja jinsi ya kuondoa wimbi sugu la udhalilishaji wanawake na watoto na hata watu wazima na kuhakikisha kila mmoja anahusika katika mapambano ya kuondoa udhalilishaji wa kijinsia ..
Nae mshiriki wa mdahalo huu Shadida Machano alisema wazazi wawe karibu na watoto wao na kuwalea malezi ya kirafiki ambayo yanazingatia maadili ili kumjengea mtoto uwezo wa kusema kwa kila ambalo linamtokezea .Alisema skuli ziandaliwe masomo maalumu ya stadi za maisha kwa wanafunzi wa skuli za msingi na sekondari ili kuweza kujielewa na kujihami.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya amali Zanzibar Riziki Pembe Juma akizungumza na Washiriki katika mdahalo wa wazi wa kupokea maoni ya Wananchi zidi ya mapambano ya ukatili na udhalilishaji wa Wanawake na watoto Zanzibar uliofanyika Viwanja vya Kariakoo kwa kuwataka Wazazi kuzidi kutoa mashirikiano juu ya vitendo vya udhalilishaji vinavyotokea ( kulia) Naibu waziri wa Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Wanawake na WatotoShadia Mohamed na Mshauri wa Rais wa Zanzibar masuala ya Wanawake Zainab Omar.
Waziri wa Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Wanawake na Watoto Mhe,Maudline Castico Akielezea juu ya wazazi kuwalea watoto katika maadili mazuri wa Kwanza( kulia) Katibu Mkuu Wizara ya Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Wanawake na Watoto Fatma Gharib.Bilali na Mwenyekiti wa Tume ya kurekebisha sheria Zanzibar Jaji Mshibe
Mmoja wa wachangiaji katika mdahalo wa wazi wa kupokea maoni zidi ya mapambano ya ukatili na udhalilishaji wa Wanawake na watoto Zanzibar Shadida Machano akichangia kwa kusema kuna vyuo mbali mbali vya madrasa vilivojitokeza bila ya kusajiliwa.
Baadhi ya Washiriki kutoka Taasisi mbali mbali waliohudhuria katika mdahalo wa wazi wa kupokea maoni zidi ya mapambano ya ukatili na udhalilishaji wa Wanawake na watoto Zanzibar wakifuatilia kwa umakini mdahalo huo uliofanyika Viwanja vya Kariakoo Mjini Unguja.
Picha na Maryama Kidiko – Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.
Hivyo makala MDAHALO WA WAZI WAKUPINGA UDHALILISHAJI WA WANAWAKE NA WATOTO.
yaani makala yote MDAHALO WA WAZI WAKUPINGA UDHALILISHAJI WA WANAWAKE NA WATOTO. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MDAHALO WA WAZI WAKUPINGA UDHALILISHAJI WA WANAWAKE NA WATOTO. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/mdahalo-wa-wazi-wakupinga-udhalilishaji.html
0 Response to "MDAHALO WA WAZI WAKUPINGA UDHALILISHAJI WA WANAWAKE NA WATOTO."
Post a Comment