title : KALIUA WATEKELEZA AGIZO LA WAZIRI MKUU LA KUWAONDOA MAAFISA UGANI OFISINI NA KWENDA KWA WAKULIMA.
kiungo : KALIUA WATEKELEZA AGIZO LA WAZIRI MKUU LA KUWAONDOA MAAFISA UGANI OFISINI NA KWENDA KWA WAKULIMA.
KALIUA WATEKELEZA AGIZO LA WAZIRI MKUU LA KUWAONDOA MAAFISA UGANI OFISINI NA KWENDA KWA WAKULIMA.
NA TIGANYA VINCENT,TABORA
HALMASHAURI ya Wilaya Kaliua imekamilisha utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu la kuwataka Maafisa Ugani kuondoka Ofisini na kwenda vijijini ili kuwasaidia wakulima katika uboreshaji wa kilimo chao kwa ajili ya maendeleo yao na taifa.
Kauli hiyo imetolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Dkt. John Pima wakati akijibu hoja za Madiwani katika kikao cha robo ya kwanza cha Baraza la Madiwani kilichokuwa kikipitia taarifa za utekelezaji.
Alisema hivi katika Ofisi za Halmashauri hiyo wamebaki Maafisa Kilimo wawili ambao ndio wanashughuli na shughuli za makao makuu ya Halmashauri na kuratibu wa mambo mengine yanayohusu masuala ya kilimo kupitia wilaya.Dkt. Pima aliowaomba Madiwani kuhakikisha wanawasimamia na kufuatilia utendaji wao wa Maafisa hao katika Kata zao ili waweze kutoa huduma na ushauri mzuri kwa wakulima kwa ajili ya kuwafanya wazalishe mazao yenye tija na manufaa kwao na kwa Halmashauri yao.
Awali Mbunge wa Jimbo la Kaliua Magdalena Sakaya alisema Halmashauri hiyo sehemu kubwa inategemea kilimo kukusanya mapato yake ya ndani na kuwataka kuwa karibu na wakulima kwa ajili ya kushauri na kuwasimamia ili waweze na uzalisjai mzuri.Alisema msimu wa kilimo kilichopita wakulima hawakuweza kufanya vizuri kutokana na mazao yakiwemo mahindi kushambuliwa na wadudu na hivyo kujikuta wakiapata mavunoa hafifu kinyume cha matarajio yao.
Sakaya alisisitiza kuwa uwepo wa karibu wa Maafisa ugani hoa kwa wakulima kutawawezesha kujua mapema matatizo wanayokabiliana nao na kuyatatua.Upelekeji wa Maafisa kilimo vijijni ni mkakati wa wilaya hiyo wa kuinua kilimo na pia unatekeleza agizo la Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa alilolitoa akiwa mkoani Tabora la kuwataka watendaji hasa wanahusika moja kwa moja na wananchi kuwafuata na kuwasaidia kutatua matatizo yao.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Haruna Kasele akifungua kikao cha kujadili taarifa za utekelezaji wa robo mwaka wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani jana.
Hivyo makala KALIUA WATEKELEZA AGIZO LA WAZIRI MKUU LA KUWAONDOA MAAFISA UGANI OFISINI NA KWENDA KWA WAKULIMA.
yaani makala yote KALIUA WATEKELEZA AGIZO LA WAZIRI MKUU LA KUWAONDOA MAAFISA UGANI OFISINI NA KWENDA KWA WAKULIMA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KALIUA WATEKELEZA AGIZO LA WAZIRI MKUU LA KUWAONDOA MAAFISA UGANI OFISINI NA KWENDA KWA WAKULIMA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/kaliua-watekeleza-agizo-la-waziri-mkuu.html
0 Response to "KALIUA WATEKELEZA AGIZO LA WAZIRI MKUU LA KUWAONDOA MAAFISA UGANI OFISINI NA KWENDA KWA WAKULIMA."
Post a Comment