title : KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA APOKEA MISAADA YA KIBINADAMU YA WAFUNGWA GEREZA KUU KARANGA, MOSHI
kiungo : KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA APOKEA MISAADA YA KIBINADAMU YA WAFUNGWA GEREZA KUU KARANGA, MOSHI
KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA APOKEA MISAADA YA KIBINADAMU YA WAFUNGWA GEREZA KUU KARANGA, MOSHI
Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Phaustine Kasike akisalimiana na Meneja Miradi wa Asasi ya Kidini ya New Life In Christ Ndg. Charles Shang’a mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Gereza Kuu Karanga Moshi kwa ajili ya hafla fupi ya kupokea Misaada ya Kibinadamu iliyotolewa na Asasi hiyo kwa ajili ya wafungwa leo Septemba 8, 2018.
Na Deodatus Kazinja, Moshi
Wito umetolewa kwa Asasi mbalimbali za kiraia nchini kujitokeza kushirikiana na Jeshi la Magereza katika kukabiliana na baadhi ya changamoto zinazoweza kulikwamisha katika kutoa huduma muhimu za wafungwa magerezani kutokana na ufinyu wa bajeti.
Hayo yamesemwa leo na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini Phaustine Kasike katika hafla ya kupokea msaada wa Kibinadamu uliotolewa na Asasi ya Kidini ya New Life In Christ iliyofanyika katika viwanja vya Gereza Kuu Karanga mjini Moshi jana Septemba 8, 2018.
“Ni ukweli usiopingika kuwa Jeshi la Magereza limekuwa likishindwa kutekeleza kwa ukamilifu utoaji wa baadhi ya huduma muhimu kwa wafungwa kutokana na ufinyu wa bajeti.” Amesema Kamishna Jenerali Kasike.
Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Phaustine Kasike (wa pili kushoto) akipokea msaada wa vifaa vya kuchomelea akiwa ni sehemu ya vifaa vilivyotolewa na Asasi ya Kidini ya New Life In Christ kwa ajili ya wafungwa vitakavyotumika kuwafundisha stadi mbalimbali za ufundi magerezani.
Jenerali Kasike ametoa wito kwa Asasi nyingine kuiga mfano uliooneshwa na New Life in Christ na Dorcas Aid International Tanzania zinavyoshirikiana na Jeshi la Magereza.
Asasi ya Kidini ya New Life In Christ pamoja na Dorcas Aid International Tanzania kwa miaka 14 sasa tangu 2005 zimekuwa zikishirikiana na Jeshi la Magereza kwa kutoa misaada ya Kibinadamu na Kiroho yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.7 hadi hivi sasa.
Kwa kipindi chote hicho Asasi hizi zimekuwa zikitoa huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na uwezeshaji wa semina za ushauri pamoja na mafunzo ya ufundi stadi kwa wafungwa na Maafisa wa Jeshi la Magereza.
Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Phaustine Kasike akipokea msaada wa vyerehani uliotolewa na Asasi ya Kidini ya New Life In Christ leo Septemba 8, 2018 kwa ajili ya wafungwa. Hafla ya upokeaji wa misaada hiyo imefanyika katika gereza Kuu Karanga Moshi.
Huduma nyingine ambazo zimewezeshwa na Asasi hizo ni kuwa na vituo vidogo vidogo vya kujifunza kufanya mambo ambayo tayari yanafanyika ndani ya magereza kama vile uokaji mikate, ushonaji na kudarizi, ushonaji wa viatu, ukinyozi, useremala na uchomeleaji mchanganyiko.
Katika hafla hiyo Asasi ya Kidini ya New Life In Christ imekabidhi msaada wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 200.2 ambapo wameahidi kuendelea kutoa misaada ya namna hiyo kwa kadiri Mungu atakavyowajalia. Misaada ya Kibinadamu iliyotolewa leo imewalenga zaidi wafungwa walioko Mikoa ya Kilimanjaro, Tanga, Arusha na Mwanza.
Wakati huo huo, Kamishna Jenerali Kasike amewaagiza wakuu wote wa magereza yote ambayo vifaa hivyo vitapelekwa kuhakikisha wanavitunza na kuvitumia kwa uadilifu kama ilivyokusudiwa.
Hivyo makala KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA APOKEA MISAADA YA KIBINADAMU YA WAFUNGWA GEREZA KUU KARANGA, MOSHI
yaani makala yote KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA APOKEA MISAADA YA KIBINADAMU YA WAFUNGWA GEREZA KUU KARANGA, MOSHI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA APOKEA MISAADA YA KIBINADAMU YA WAFUNGWA GEREZA KUU KARANGA, MOSHI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/kamishna-jenerali-wa-magereza-apokea.html
0 Response to "KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA APOKEA MISAADA YA KIBINADAMU YA WAFUNGWA GEREZA KUU KARANGA, MOSHI"
Post a Comment