title : HIVI HAPA VYUO VIKUU VINAVYOPENDWA NA WAAJIRI AFRIKA.
kiungo : HIVI HAPA VYUO VIKUU VINAVYOPENDWA NA WAAJIRI AFRIKA.
HIVI HAPA VYUO VIKUU VINAVYOPENDWA NA WAAJIRI AFRIKA.
Shahada ya chuo kikuu gani Afrika ambayo inapendelewa na waajiri zaidi duniani? Afrika Mashariki kuna chuo kikuu kimoja pekee, vyuo vikuu vingine vikitoka Afrika Kusini na Misri.Hii ni kwa mujibu wa utafiti wa 'Kuajirika kwa Wanaofuzu na Shahada Duniani wa 2019' ambao umefanywa na kampuni ya QS Group na huwa kiashiria cha matumaini ambayo wanafunzi wanaweza kuwa nayo wakitafuta kazi baada ya kufuzu.
Orodha ya sasa imetayarishwa baada ya kutafuta maoni ya waajiri 42,000 kote duniani na ni kiashiria cha chuo kikuu gani kinapendwa zaidi na waajiri.
Waajiri waliulizwa kuhusu ni wapi watu wenye shahada walio na "ujuzi zaidi, ubunifu na uvumbuzi na wanaomudu kazi vyema zaidi" hutoka.
Orodha hiyo pia huzingatia takwimu za idadi ya wanafunzi waliohitimu vyuo mbalimbali ambao huajiriwa, ni wapi watu wenye vyeo vya juu mashirika mbalimbali walisomea na pia ushirikiano uliopo baina ya vyuo vikuu na waajiri mbalimbali.
Kwa jumla duniani, Massachusetts Institute of Technology (MIT) ndicho chuo kikuu kinachoongoza.
Vyuo vikuu vya Marekani vinashikilia nafasi nne za kwanza MIT, Stanford, University of California, Los Angeles (UCLA), na Harvard, ambapo wanafunzi wake hutafutwa zaidi na waajiri.
Stanford, wanashikilia nafasi ya pili na wamekuwa ndio kitovu cha wasomi wengi wanaoangazia na kutafiti kuhusu uvumbuzi Silicon Valley. Wanafunzi wa zamani ni kama vile waanzilishi wa Google Larry Page na Sergey Brin na mwanzilishi wa Netflix Reed Hastings.
Orodha hiyo inaonesha vyuo vikuu vya Australia vimeanza kuimarika, ambapo University of Sydney na University of Melbourne vinashikilia nafasi ya tano na sita mtawalia.
Vyuo hivyo havijawahi kujumuishwa katika vyuo vikuu 30 bora katika Orodha ya Vyuo Vikuu Bora Duniani ya QS, lakini vinaonekana kupendwa sana na waajiri.
Ben Sowter, mkurugenzi wa utafiti katika QS, anasema vyuo vikuu vinavyosifika kwa utafiti duniani si lazima viwe ndivyo vinavyopendwa na waajiri.
Amesema pia kwamba gharama ya karo na ushindani sokoni vimesababisha wanafunzi kuangazia zaidi uwezekano wao kuajiriwa baada ya masomo na mafanikio yao ya baadaye.
Cambridge ndicho chuo kikuu cha Uingereza kilichoorodheshwa cha juu zaidi katika nafasi ya 10.
College London ni cha 18. Kwa kuangazia sifa za vyuo vikuu miongoni mwa waajiri, Cambridge na Oxford ndivyo vinavyoongoza, lakini kwa jumla vyuo vikuu vya Uingereza vilishuka katika ushirikiano na waajiri na viwango vya . kwa wanafunzi wao.
Kuimarika kwa China kunadhihirishwa na kuorodheshwa kwa Tsinghua University nafasi ya tisa na University of Peking nafasi ya 20
ghorofa Marekani?
Kati ya vyuo vikuu 500 vilivyoorodheshwa, 102 vinatoka bara Asia, 144 kutoka Ulaya Magharibi. Marekani ina vyuo vikuu 83, ambapo 13 kati ya vyuo hivyo vimo katika orodha ya 30 bora. Afrika kuna vyuo vikuu 10.
Chuo hicho kikuu cha Nairobi ndicho pekee kutoka Afrika Mashariki ingawa kimeshuka kutoka nambari tano Afrika mwaka 2018, mwaka ambao kulikuwa na vyuo vikuu 11 vya Afrika katika vyuo vikuu 500 bora duniani kwenye orodha hiyo.
Vyuo Vikuu vinavyopendwa na waajiri Afrika 2019.
University of Cape Town, Afrika KusiniThe American University in Cairo, MisriUniversity of Witwatersrand, Afrika KusiniCairo University, MisriAin Shams University, MisriStellenbosch University, Afrika KusiniUniversity of Johannesburg, Afrika KusiniUniversity of Kwazulu-Natal, Afrika KusiniUniversity of Nairobi, KenyaUniversity of Pretoria, Afrika Kusini
Chuo kikuu cha Alexandria cha Misri ndicho kilichotupwa nje katika orodha ya mwaka huu baada ya kuwa nambari nane Afrika mwaka uliopita.
Chuo kikuu cha Cape Town ambacho kinaongoza Afrika katika orodha ya jumla kinashikilia nafasi ya 101-110, na hakuna chuo kingine cha Afrika hadi baada ya vyuo mia ambapo ndipo unapata chuo kikuu cha Kimarekani cha Cairo na Chuo Kikuu cha Witwatersrand cha Afrika Kusini katika nafasi ya 201-250.
Chuo Kikuu cha Nairobi kinashikilia nafasi ya 301-500. Mwaka jana, kilikuwa katika nafasi ya 251-300 kwa jumla.
Mwaka 2017, Afrika ilikuwa na vyuo vikuu vinne pekee, wakati huo orodha hiyo kwa jumla ikishirikisha vyuo vikuu 300 duniani. Mwaka 2017 walishirikisha vyuo 494 na mwaka huu vyuo 497.
Hivyo makala HIVI HAPA VYUO VIKUU VINAVYOPENDWA NA WAAJIRI AFRIKA.
yaani makala yote HIVI HAPA VYUO VIKUU VINAVYOPENDWA NA WAAJIRI AFRIKA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala HIVI HAPA VYUO VIKUU VINAVYOPENDWA NA WAAJIRI AFRIKA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/hivi-hapa-vyuo-vikuu-vinavyopendwa-na.html
0 Response to "HIVI HAPA VYUO VIKUU VINAVYOPENDWA NA WAAJIRI AFRIKA."
Post a Comment