title : GULAMALI AENDELEA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA NA ELIMU MANONGA
kiungo : GULAMALI AENDELEA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA NA ELIMU MANONGA
GULAMALI AENDELEA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA NA ELIMU MANONGA
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MBUNGE wa Manonga Mh. Seif Khamis Gulamali ameendelea na ziara yake jimboni humo katika kukagua na kuangalia namna miradi ya maendeleo inavyoendelea kutekelezwa kunufaisha wana Manonga.
Katika ziara ziara yake Gulamali alitembelea kituo cha afya Simbo sambamba na kukagua ujenzi wa madarasa matatu katika shule ya sekondari Mwisi ambako ameridhishwa namna miradi hiyo inavyotekelezwa na kuwataka wasimamizi kwenda na kasi na kufanya kazi zilizo bora zaidi.
Aidha Mbunge huyo alipata wasaa wa kukutana na kamati ya Zahanati ya Nkinga, viongozi wa CCM na wadau wengine na kuona namna ukarabati wa miundombinu katika Zahanati ya Nkinga unavyoendelea.
Gulamali ameahidi kutoa kiasi cha shilingi 430,000 kwa ajili ya kuvuta maji ya Uhakika kwenye Zahanati ya Nkinga ili kupunguza adha kwa wananchi wa wauguzi katika mchakato mzima wa kutoa na kupokea huduma.
Pia ameahidi kuongeza vitanda viwili vya kujifungulia katika wodi ya wazazi na kueleza kuwa suala la afya hasa ya mama na mtoto lazima ipewe kipaupele.
Gulamali alihitimisha ziara yake kwa kufanya kikao na wachezaji pamoja na viongozi wa timu ya Manonga Queens ambayo iliibuka kidedea kwa kuichapa Singida Worrier kwa goli mbili, na amekabidhi mipira miwili na kuahidi jezi na vifaa vya michezo ambavyo ameshaagiza kwa ajili ya timu hiyo itakayowakilisha mkoa mzima wa Tabora kwenye michuano ya soka daraja la kwanza Tanzania bara kwa timu za wanawake.

Mbunge wa Manonga Seif Gulamali (katikati) akizungumza na kamati ya Zahanati ya Nkinga mara baada ya kuwasili.
Hivyo makala GULAMALI AENDELEA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA NA ELIMU MANONGA
yaani makala yote GULAMALI AENDELEA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA NA ELIMU MANONGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala GULAMALI AENDELEA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA NA ELIMU MANONGA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/gulamali-aendelea-kuboresha-huduma-za.html
0 Response to "GULAMALI AENDELEA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA NA ELIMU MANONGA"
Post a Comment