title : Serikali Yaandaa Mtaala Utakaotumika Kuwanoa Wanasheria Wapya
kiungo : Serikali Yaandaa Mtaala Utakaotumika Kuwanoa Wanasheria Wapya
Serikali Yaandaa Mtaala Utakaotumika Kuwanoa Wanasheria Wapya
Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) Chadhamiria Kuwajengea Uwezo waajiriwa wapya Serikalini wa Kada ya Sheria ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi.
Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt . Laurean Ndumbaro wakati akifungua Kongamano la Wadau lililolenga kupitia na kutoa maoni kuhusu mtaala wa mafunzo elekezi kwa mawakili na wanasheria wa sekta ya umma, Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Mick Kiliba amesema kuwa lengo ni kuwajengeauwezo wanasheria hao ili waweze kujua mifumo ya uendeshaji wa shughuli za Serikali, Uongozi na Utumishi wa Umma.
“Lengo la kuwaandaa waajiriwa wapya wa Kada ya Sheria ni kujenga utumishi uliotukuka na bora katika Kada hii muhimu kwa maendeleo ya Taifa letu”; Alisisitiza Kiriba.Akifafanua Bw. Kiliba amesema kuwa waraka namba (5) Tano wa mwaka 2011 wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, unaoelekeza kutolewa kwa mafunzo elekezi kwa watumishi wapya katika Utumishi wa Umma.
Aliongeza kuwa Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto kimekasimiwa madaraka ya kuandaa na kutoa mafunzo ya awali na elekezi kwa waajiriwa wote wa kada ya Sheria katika sekta ya Umma nchini.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais; Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Mick Kiliba akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Dkt. Laurean Ndumbaro leo Jijini Dodoma wakati wa hafla ya ufunguzi wa kongamano la wadau kutoa maoni kuhusu mtaala wa mafunzo elekezi kwa wanasheria wapya kwenye Utumishi wa Umma.Kongamano hilo limeandaliwa na Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.
Mkuu wa Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto Mhe. Jaji Paul Kihwelo (PhD) akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa kongamano la wadau kutoa maoni kuhusu mtaala wa mafunzo elekezi kwa wanasheria wapya kwenye Utumishi wa Umma leo Jijini Dodoma.
Mkuu wa Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto Mhe. Jaji Paul Kihwelo (PhD) akisisitiza jambo kwa washiriki wa kongamano la wadau kutoa maoni kuhusu mtaala wa mafunzo elekezi kwa wanasheria wapya kwenye Utumishi wa Umma leo Jijini Dodoma.
Hivyo makala Serikali Yaandaa Mtaala Utakaotumika Kuwanoa Wanasheria Wapya
yaani makala yote Serikali Yaandaa Mtaala Utakaotumika Kuwanoa Wanasheria Wapya Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Serikali Yaandaa Mtaala Utakaotumika Kuwanoa Wanasheria Wapya mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/serikali-yaandaa-mtaala-utakaotumika.html
0 Response to "Serikali Yaandaa Mtaala Utakaotumika Kuwanoa Wanasheria Wapya"
Post a Comment