title : DC BAGAMOYO AKUTANA NA WAFUGAJI KATA YA VIGWAZA KWA AJILI YA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI
kiungo : DC BAGAMOYO AKUTANA NA WAFUGAJI KATA YA VIGWAZA KWA AJILI YA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI
DC BAGAMOYO AKUTANA NA WAFUGAJI KATA YA VIGWAZA KWA AJILI YA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI
Mkuu wa Wilaya ya Bgamoyo wa kushoto alipowatembea wafugaji wa kimasai katika mnada wa kuuza mbuzi na ng’ombe katika kijiji cha Chamakweza.
VICTOR MASANGU, VIGWAZA
KATIKA kukabiliana na wimbi la uvunjifu wa amani katika halmashauri ya Chalinze unaochangiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na migogoro ya ardhi baina na wakulima na wafugaji hatimaye Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa ameingilia kati sakata hilo kwa kuamua kukutana na jamii ya wafugaji kwa lengo la kuweza kulitafutia ufumbuzi wa kina ili kumaliza kabisa changamoto ya kutokea kwa mapigano.
Mkuu huyo wa Wilaya akizungumza na wafugaji hao kutoka vijiji mbali mbali vilivyopo katika kata ya Vigwaza katika mkutano wa hadhara ambao aliuandaa maalumu kwa lengo la kuweza kusuluhisha migogoro iliyopo pamoja na kusikiliza kero na changamoto mbali mbali ambazo zinawakabili jamii ya wafugaji na ili kuweza kuzitatua.
Aidha mkuu huyo alisema kwamba amesikitisha sana tukio lililotokea hivi karibu katika kijiji cha Pongwe ambapo mkulima mmoja kupoteza maisha baada ya kuchomwa na mkuki kifuani kutokana na ugomvi wa kugombania ardhi, hivyo ameahidi kutoa ushirikiano wa dhati katika pande zote mbili na kuwataka wananchi kuwafichua watu ambao wanahusika katika kuchochea migogoro hiyo na ambao wanahusika katika matukio hayo ya mauaji ili waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
Wafugaji ambao ni jamii ya kimasai kutoka kata ya vigwaza wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo katika mkutano huo wa hadhara.
Pia katika hatua nyingine alibainisha kwamba lengo la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inamaliza tofauti zote baina ya wakulima na wafugaji na kuwataka kuheshimiana na kuepukana na masuala ya mapigano na badala yake watekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria na taratibu zote za nchi ili kuondokana kabisa na migogoro iliyopo.
Naye Makamu Mwenyekiti wa chama cha wafugaji Tanzania Ester Moleta ameiomba serikali ya awamu ya tano kuhakikisha kwamba inawasaidia kwa ahali na mali kuwapatia elimu juu ya ufugaji bora wa mifugo pamoja na kujifunza sheria na taratibu mbali mbali za matumizi bora ya ardhi kwa lengo la kuweza kuondokana na matatizo ya migogoro ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara kati ya wakulima na wafugaji.
Hama kwa upande mmoja wa wafugaji hao akizungumza kwa niba ya wenzake ambaye pia ni Katibu mkuu mstaafu wa chama cha wafugaji Tanzania (CCWT) George Kifuko amesema kwamba migogoro mingi inayojitokeza inasababishwa na baadhi ya viongozi wa vijiji na vitongoji kuamua kujiuzia maeneo kiholela kinyume kabisa na taratibu na sheria zilizowekwa hivyo ni vema pindi watakapobainika wakachukulia hatua kali ili iwe fundisho kwa wengine.
HALMASHAURI ya Chalinze iliyopo Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani imekuwa ikikabiliwa na changamoto kubwa kwa kipindi cha muda mrefu kutokana na kuibuka kwa migogoro ya kugombania maeneo ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji ambayo inasababisha kutokea kwa uvunjifu wa amani hivyo jitahada za mkuu wa Wilaya kuzungumza na pande zote mbili kutaweza kusaidia kusuluhisha.
Hivyo makala DC BAGAMOYO AKUTANA NA WAFUGAJI KATA YA VIGWAZA KWA AJILI YA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI
yaani makala yote DC BAGAMOYO AKUTANA NA WAFUGAJI KATA YA VIGWAZA KWA AJILI YA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC BAGAMOYO AKUTANA NA WAFUGAJI KATA YA VIGWAZA KWA AJILI YA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/dc-bagamoyo-akutana-na-wafugaji-kata-ya.html
0 Response to "DC BAGAMOYO AKUTANA NA WAFUGAJI KATA YA VIGWAZA KWA AJILI YA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI"
Post a Comment