title : Bodi ya Korosho Yashauriwa Kuzitumia Taasisi za Kijeshi za JKT Mgambo na JKT Maramba Mchakato wa Uzalishaji wa Miche ya Mikorosho.
kiungo : Bodi ya Korosho Yashauriwa Kuzitumia Taasisi za Kijeshi za JKT Mgambo na JKT Maramba Mchakato wa Uzalishaji wa Miche ya Mikorosho.
Bodi ya Korosho Yashauriwa Kuzitumia Taasisi za Kijeshi za JKT Mgambo na JKT Maramba Mchakato wa Uzalishaji wa Miche ya Mikorosho.
BODI ya korosho Mkoa Tanga imeshauriwa kuzitumia taasisi za Kijeshi za JKT Mgambo na JKT Maramba ili ziweze kusaidia katika mchakato wa uzalishaji wa miche ya mimea hiyo ya korosho.
Hayo yamezungumzwa na Mkuu wa Mkoa Tanga Martin Shigella kwenye mkutano wa wadau wa zao la korosho uliokuwa na lengo la kujadili maendeleo ya Tasnia ya zao la korosho kwa kipindi cha msimu wa miaka mitatu.
Shigella alisema ili bodi hiyo iweza kukabiliana na uhaba wa miche katika Halmashauri zinazolima zao hilo lazima ifike wakati taasisi hizo ziweze kutumika kukabidhiwa mbegu kwa ajili ya kuzalisha miche hiyo.
“Jaribuni kuwasiliana na taasisi hizio za kijeshi ambazo wanawataalamu wa kuandaa vitalu wanaweza kuwasaidia kuzalisha miche mingi na iliyo na ubora unaotakiwa”Alisema Shigella.
Mbali na hilo pia alizitaka Halmashauri zote zinazolima zao hilo kuhakikisha zinatenga bajeti mapema ndani ya mwezi huu wa Sept kwa ajili ya ununuzi wa mbegu toka katika Taasisi ya Utafiti wa kilimo(Naliendele) kwa ajili ya uzalishaji wa miche ambayo inatarajiwa kusambazwa mwakani kwa wakulima wote
Awali akizungumzi suala hilo Meneja Bodi ya korosho Kanda ya Kaskazini Mashariki Ugumba Kilasa alikiri umuhimu wa kuzitumia taasisi hizo kutokana na na uhaba wa fedha zilizokuwa zinatumika kuvilipa vikundi vinavyozalisha miche hiyo.
Kilasa alisema lengo ni mjadala wa kuongeza uzalishaji wa zao hilo Mkoani hapa na ongezeko hilo lazima liendende sambamba na uwepo wa miche mipya,bora na ya kisasa jambo ambalo ikiwa kutaanzishwa vitalu vya kukuzia miche na taasisi hizo hali ya uzalishaji inaweza kubadilika.
“Awali tulikuwa na vikundi vya vijana tuliokuwa tunawatumia kuzalisha miche hiyo na tulikuwa tunawalipa lakini kutokana na ufinyu wa fedha ni bora tutumie taasisi hizo za JKT zitatusaidia”Alisema Kilasa.
Alisema mikakati endelevu ifanyike ili kuhakikisha ongezeko la uzalishaji linakuwepo hasa kwa kupanda miche mipya itakayoweza kuzaa kwa wingi na kuongeza uchumi wa mkulima mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla
Nae Mrajisi Msaidizi vyama vya Ushirika Mkoa Tanga Jacklin Senzige alisema kweli lipo tatizo la upatikanaji wa pembejeo kwa wakati jambo ambalo linaweza kukwamisha usambazaji wake kwa wakulima na kuathiri uzalishaji kwa ujumla.
Alisema uzalishaji wa Korosho mkoani Tanga umeshuka kutoka tani 1712 mwaka 2016/2017 hadi kufikia tani 1381 mwaka 2017/2018 hali iliyosababishwa na mvua za mfululizo zilizonyesha kwa kipindi kirefu na kusababisha maua kudondoka na kuozesha matunda.
Hivyo makala Bodi ya Korosho Yashauriwa Kuzitumia Taasisi za Kijeshi za JKT Mgambo na JKT Maramba Mchakato wa Uzalishaji wa Miche ya Mikorosho.
yaani makala yote Bodi ya Korosho Yashauriwa Kuzitumia Taasisi za Kijeshi za JKT Mgambo na JKT Maramba Mchakato wa Uzalishaji wa Miche ya Mikorosho. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Bodi ya Korosho Yashauriwa Kuzitumia Taasisi za Kijeshi za JKT Mgambo na JKT Maramba Mchakato wa Uzalishaji wa Miche ya Mikorosho. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/bodi-ya-korosho-yashauriwa-kuzitumia.html
0 Response to "Bodi ya Korosho Yashauriwa Kuzitumia Taasisi za Kijeshi za JKT Mgambo na JKT Maramba Mchakato wa Uzalishaji wa Miche ya Mikorosho."
Post a Comment