title : ZIWA SINGIDANI NA KINDAI KUTANGAZWA KAMA MAENEO LINDWA KIMAZINGIRA
kiungo : ZIWA SINGIDANI NA KINDAI KUTANGAZWA KAMA MAENEO LINDWA KIMAZINGIRA
ZIWA SINGIDANI NA KINDAI KUTANGAZWA KAMA MAENEO LINDWA KIMAZINGIRA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akifafanua vifungu vya Sheria ya Mazingira mbele ya Watendaji na Viongozi wa Mkoa wa Singida juu ya maeneo lindwa. Wengine katika picha ni viongozi wa Mkoa wa Singida wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Rehema Nchimbi (wa pili kutoka kushoto).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akijionea uharibifu wa mazingira katika Ziwa Singidani ambao unatokana na shughuli za kibinadamu. Waziri Makamba ameazimia kunusuru Ziwa hilo pamoja na vyanzo vyake. Wengine katika picha ni viongozi kutoka Manispaa ya Singida.
Ziwa Singidani ambalo liko hatarini kutoweka kutokana na shughuli zisizo endelevu za kibinadamu. Waziri Makamba yuko katika ziara ya kikazi ya kukagua na kuona namna bora ya kunusuru Ziwa hilo pamoja na mengine kwa mustakabali wa nchi yetu.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe.
January Makamba amesema Ofisi yake inaangalia uwezekano wa kutangaza
Ziwa Singidani na Ziwa Kindai katika Halmashauri ya Singida kama maeneo
lindwa kimazingira kwa kuwa yako hatarini kutoweka.
Waziri Makamba ameyasema hayo hii leo Mkoani Singida ikiwa ni siku ya
kwanza ya ziara yake katika Mikoa 9 hapa nchini yenye lengo kukagua,
kutathmini na kuzungumza na viongozi, wataalam, watendaji na wananchi
kuhusu maeneo yanayopendekezwa kuhifadhiwa kwa mujibu wa Sheria ya
Mazingira kifungu namba 51.
Aidha, Waziri Makamba amesema kuwa mara baada ya kutoa tangazo hilo
katika gazeti la Serikali matumizi sahihi ya maziwa hayo yataainishwa ikiwa nipamoja na kupanda miti rafiki kuzunguka maeneo yote na kuzingatia makatazo yatakayotolewa.
“Ziwa Singidani liko hatarini kutoweka kutona na shughuli za kibinadamu,
hivyo kwa kutumia Sheria ya Mazingira nitashauriana na wataalamu wangu
kuona namna bora ya kunusuru maziwa haya ikiwa ni pamoja na
kuyatangaza kwenye gazeti la Serikali kama maeneo lindwa kimazingira.”
Makamba alisisitiza.
Imebainika kuwa, lengo la kuainisha na kutangaza maeneo hayo ni kulinda
mifumo muhimu ya kiikolojia (ikiwemo vyanzo vya maji, mito, maziwa,
mabwawa, milima na vilima, chemichemi, ardhi oevu, mazalia ya samaki na
misitu) ambayo hayana ulinzi wa Sheria nyingine.
Waziri Makamba pia ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Singida kwa utayari na uwezo wao katika kusimamia uhifadhi mara maeneo hayo
yatakapotangazwa na kuwataka kuwasiliana na Ofisi yake ili waweze
kupatiwa rasimu ya Sheria ndogo ndogo watakazozitumia katika Halmashauri zao ili kukabiliana na changamoto za uharibifu wa mazingira katika ngazi zote.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amesema Mkoa wake
uko tayari kuingia makubaliano na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) yenye lengo la kuhuisha Sheria ndogo ndogo
zitakazosaidia hifadhi ya Mazingira mkoani kwake pamoja na kuundwa kwa
Kamati za Mazingira katika ngazi zote.
Jumla ya maeneo 77 yamependekezwa kutoka Mikoa mbalimbali kwa
kuzingatia vigezo vilivyowekwa kwa mujibu wa Sheria na katika awamu ya
kwanza, maeneo takriban 20 yanatarajiwa kuhifadhiwa kwa kutumia Sheria ya Mazingira.
Hivyo makala ZIWA SINGIDANI NA KINDAI KUTANGAZWA KAMA MAENEO LINDWA KIMAZINGIRA
yaani makala yote ZIWA SINGIDANI NA KINDAI KUTANGAZWA KAMA MAENEO LINDWA KIMAZINGIRA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ZIWA SINGIDANI NA KINDAI KUTANGAZWA KAMA MAENEO LINDWA KIMAZINGIRA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/ziwa-singidani-na-kindai-kutangazwa.html
0 Response to "ZIWA SINGIDANI NA KINDAI KUTANGAZWA KAMA MAENEO LINDWA KIMAZINGIRA"
Post a Comment