title : Yanga sc,Mtibwa Sugar vuta ni kuvute katika dimba la Taifa
kiungo : Yanga sc,Mtibwa Sugar vuta ni kuvute katika dimba la Taifa
Yanga sc,Mtibwa Sugar vuta ni kuvute katika dimba la Taifa
Na Agness Francis, Globu ya jamii.
IKIWA imebaki masaa machache tu kikosi cha Yanga kushuka dimbani katika mchezo wao wa kwanza wa ligi kuu Tanzania bara msimu huu 2018-19.
Mabingwa hao wa kihistoria mara 27 watamenyana na wakatamiwa wa mkoa wa Morogoro mtibwa sugar, ambapo msimu huu ligi inatarajia kuwa na ushindani kutokana na maandalizi yaliyofanywa kwa kila kikosi, vilevile pia ongezeko la timu kutokea 16 hadi 20 litaleta msisimko.
Yanga iliyoweka kambi ya wiki mbili Mkoani Morogoro imerejea upya kwa nguvu zaidi baada ya kuichapa USM Alger mabao 2-1 katika mchezo wa wa Kombe la shirikisho,ambapo magoli ya Yanga yalifungwa na Deus Kaseke pamoja na Heritier Makambo mchezaji nyota raia wa Kongo.
Msimu uliopita kikosi cha Yanga kilikuwa na wakati mgumu kwa wachezaji wake waandamizi kuwa majeruhi wa mara kwa mara kwa wacheza mpaka kupelekea timu kushiriki mashindano mengi ikiwa na kikosi finyu.
"Sipendi kuliona hilo litokee tena msimu huu, nitaakikisha angalau asilimia 80% ya wachezaji wanakuwa na utimamu wa kimwili na naamini kutwaa ubingwa msimu huu kwa kuwa kikosi changu kipo vizuri na kipana"amesema kocha mkuu Zahera raia wa Kongo.
Wachezaji wa yanga watakaokuwa sehemu ya mchezo huo dhidi mtibwa ni 1 Claus Kindoki,2Juma Abdu,3Gadiel Michael,4Vicent Andrew,5Kelvin Yondan,6Papy Kabamba,7Mrisho Ngasa,8 Feisal Aballa (Fei toto),9Heritier Makambo,10 Ibrahim Ajibu, pamoja na Deus Kaseke anaevalia jezi namba 11.
Mchezo huo unatarajia kuchezwa leo majira ya Saa 12jioni katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kwa kiingilio cha VIP A 10000,VIP B 3000,na kwa viti vingine vilivyobaki ni 1500.
Hivyo makala Yanga sc,Mtibwa Sugar vuta ni kuvute katika dimba la Taifa
yaani makala yote Yanga sc,Mtibwa Sugar vuta ni kuvute katika dimba la Taifa Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Yanga sc,Mtibwa Sugar vuta ni kuvute katika dimba la Taifa mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/yanga-scmtibwa-sugar-vuta-ni-kuvute.html
0 Response to "Yanga sc,Mtibwa Sugar vuta ni kuvute katika dimba la Taifa"
Post a Comment