title : AZAM YAPANGA KUANZA NA USHINDI DHIDI YA MBEYA CITY
kiungo : AZAM YAPANGA KUANZA NA USHINDI DHIDI YA MBEYA CITY
AZAM YAPANGA KUANZA NA USHINDI DHIDI YA MBEYA CITY
KOCHA Mkuu wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Hans Van Der Pluijm, ameelezea mikakati yake kuelekea mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) dhidi ya Mbeya City.
Mholanzi huyo wakati amesema kuwa jambo la muhimu ni kikosi chake kuanza vema msimu wa ligi kesho Alhamisi kwa kuibuka na ushindi dhidi ya timu hiyo yenye maskani yake jijini Mbeya, mchezo utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex saa 2.00 usiku.
“Maandalizi yetu kuelekea ligi yamefanyika vizuri matarajio yetu ni makubwa nadhani sio kwetu tu ni kwa kila mtu hadi hivi sasa tuna majeruhi wawili ambao hawawezi kuwepo kwenye mechi ya kwanza watakaokuwepo kwenye mechi zinazofuata lakini nafikiri tunatimu nzuri.
“Ninachojua kuhusu Mbeya City, siku zote wamekuwa wapinzani wagumu, sio tu wanapokutana na Azam FC au Simba au Yanga daima wamekuwa wakionyesha zaidi kuliko wanavyoonyesha mechi nyingine lakini najua kitu cha kufanya na ndio maana nipo hapa, tunatarajia mchezo mgumu,” alisema Pluijm.
Azam FC itaingia kwenye msimu mpya wa ligi ikiwa na morali kubwa baada ya kutwaa ubingwa wa pili mfululizo wa michuano ya Kombe la Kagame, ikiifunga Simba mabao 2-1, yaliyofungwa na mshambuliaji Shaaban Idd, aliyehamia CD Tenerife ya Hispania na nahodha Agrey Moris, aliyefunga la ushindi akizima bao lililosawazishwa na Meddie Kagere.
Kocha huyo wa zamani wa Berekum Chelsea, Ashanti Gold za Ghana, Singida United na Yanga, alisema ugumu wa mchezo huo sio kitu kwani kila mechi si sawa akidai anaamini wataibuka na ushindi baada ya dakika 90.
“Cha muhimu ni timu yetu kucheza kwa mpangilio na kutofanya makosa na kutumia nafasi tunazopata na mwisho wa siku baada ya dakika 90 naamini tutaibuka na ushindi,” alisema.
Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana ndani ya Azam Complex, Azam FC iliibuka kidedea kwa ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na mshambuliaji Mbaraka Yusuph.
Hivyo makala AZAM YAPANGA KUANZA NA USHINDI DHIDI YA MBEYA CITY
yaani makala yote AZAM YAPANGA KUANZA NA USHINDI DHIDI YA MBEYA CITY Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala AZAM YAPANGA KUANZA NA USHINDI DHIDI YA MBEYA CITY mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/azam-yapanga-kuanza-na-ushindi-dhidi-ya.html
0 Response to "AZAM YAPANGA KUANZA NA USHINDI DHIDI YA MBEYA CITY"
Post a Comment