title : Waziri Mwakyembe Atoa Miezi 3 kwa Maafisa Utamaduni kukamilisha Ukusanyaji Maoni Ya Sera
kiungo : Waziri Mwakyembe Atoa Miezi 3 kwa Maafisa Utamaduni kukamilisha Ukusanyaji Maoni Ya Sera
Waziri Mwakyembe Atoa Miezi 3 kwa Maafisa Utamaduni kukamilisha Ukusanyaji Maoni Ya Sera
Na Anitha Jonas – WHUSM- Marangu Kilimanjaro – Moshi
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe amewataka Maafisa Utamaduni Mkoa na Wilaya kuwahimiza wadau wa Sekta ya Utamaduni kuwasilisha maoni yao ndani ya miezi mitatu.
Mheshimiwa Mwakyembe ametoa kauli hiyo leo katika Kijiji cha Marangu Mkoani Kilimanjaro alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa Saba wa Umoja wa Machifu nchini wenye lengo la kujadili namna ya kuhakikisha umoja huo unasajiliwa kisheria pamoja na kuzungumzia nini kifanyike kutokana na kuwepo na mmomonyoko wa maadili katika jamii kwa kiasi kikubwa.
“Serikali iko katika mchakato wa kufanya maboresho ya Sera ya Utamaduni ya mwaka 1997 ambayo imeonekana kuwa na mapungufu kulingana na hali ilivyosasa,hivyo basi nitoe rai kwenu Machifu kama wadau wakuu wa Sekta ya Utamaduni kutoa maoni yenu kwa haraka kwani yatasaidia kwa asilimia kubwa kuongeza ubora katika sera hii tunayoboresha na hivyo basi hakikisheni mnawasilisha maoni yenu kwa Maafisa Utamaduni ndani ya miezi hiyo,”alisema Mhe.Dkt.Mwakyembe.
Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Machifu Tanzania Chifu Frank Marrialle alieleza kuwa umoja huo ulianza tangu mwaka 2014 na mpaka sasa unajumla ya wanachama 105 na kupitia umoja huo umekuwa ukisisitiza wajumbe wake kusimamia utunzaji mazingira pamoja usimamazi wa maadili katika jamii kwani machifu ndiyo mhimili wa kulinda utamaduni wa taifa.
“Mbali na Machifu hawa kujitahidi kupigania usimamizi wa maadili katika jamii zao wamekuwa wakikumbwa na changamoto nyingi kwani kwa baadhi ya maeneo wamekuwa wakitolewa maneno ya dharau na kejeli kwa kuwaelezwa kuwa utawala wao umepitwa na hauna maana kwa sasa ombi letu kwa serikali ni kuhakikisha kupitia maoni yetu tutakayowasilisha kwa ajili Sera hii ya Utamaduni inayofanyiwa marekebisho yatiliwe mkazo ili kuonyesha wa nguvu ya machifu kwa jamii,”alisema Marrialle.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe(katikati) akitoa maagizo kwa Maafisa Utamaduni Mkoa na Wilaya nchini kukamilisha ukusanyaji wa maoni ya wadau wa Sekta ya Utamaduni kwa ajili ya kuboresha Sera ya Utamaduni ya Mwaka 1997 katika ufunguzi wa Mkutano wa Saba wa Umoja wa Machifu uliyofanyika leo katika Kijiji cha Marangu Mkoani Kilimanjaro,Kushoto ni Mlezi wa Umoja wa Machifu Tanzania Waziri Mkuu Mstaafu Mhe.John Samuel Malecela na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Bi.Lilian Beleko kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Machifu Tanzania Chifu Frank Marrialle (kushoto) akitoa ahadi ya umoja huo kuwasilisha maoni yao kwa ajili ya kuboresha Sera ya Utamaduni ya Mwaka 1997 kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe(hayupo pichani) katika ufunguzi wa Mkutano wa Saba wa Umoja wa Machifu Tanzania uliyofanyika leo katika Kijiji cha Marangu Mkoani Kilimanjaro,kulia kwake ni Mlezi wa Umoja wa Machifu Tanzania Waziri Mkuu Mstaafu Mhe.John Samuel Malecela.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (kulia) akikabidhi nakala 21 za Sera ya Utamaduni ya Mwaka 1997 kwa Mlezi wa Umoja wa Machifu Tanzania Waziri Mkuu Mstaafu Mhe.John Samuel Malecela (kushoto) katika Ufunguzi wa Mkutano wa Saba wa Umoja wa Machifu Tanzania,uliyofanyika leo katika Kijiji cha Marangu Mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kugawa kwa Machifu waliyoshiriki Mkutano huo ili waweze kutoa maoni yao kutokana na mapungufu ya sera hiyo inayofanyiwa marekebisho.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe aliyeketi (watano kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Machifu wa Tanzania mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Saba wa Umoja wa Machifu Tanzania uliyofanyika leo katika Kijiji cha Marangu Mkoani Kilimanjaro,wanne kulia ni Mlezi wa Umoja wa Machifu Tanzania Waziri Mkuu Mstaafu Mhe.John Samuel Malecela,na wanne kulia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Machifu Tanzania Chifu Frank Marrialle.
Hivyo makala Waziri Mwakyembe Atoa Miezi 3 kwa Maafisa Utamaduni kukamilisha Ukusanyaji Maoni Ya Sera
yaani makala yote Waziri Mwakyembe Atoa Miezi 3 kwa Maafisa Utamaduni kukamilisha Ukusanyaji Maoni Ya Sera Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Waziri Mwakyembe Atoa Miezi 3 kwa Maafisa Utamaduni kukamilisha Ukusanyaji Maoni Ya Sera mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/waziri-mwakyembe-atoa-miezi-3-kwa.html
0 Response to "Waziri Mwakyembe Atoa Miezi 3 kwa Maafisa Utamaduni kukamilisha Ukusanyaji Maoni Ya Sera"
Post a Comment