title : WADAIWA WA MASURUFU YA SAFARI KATIKA MANISPAA YA KUKATWA KATIKA MISHAHARA YAO YA SEPTEMBA
kiungo : WADAIWA WA MASURUFU YA SAFARI KATIKA MANISPAA YA KUKATWA KATIKA MISHAHARA YAO YA SEPTEMBA
WADAIWA WA MASURUFU YA SAFARI KATIKA MANISPAA YA KUKATWA KATIKA MISHAHARA YAO YA SEPTEMBA
NA TIGANYA VINCENT-RS TABORA
BARAZA la Madiwani limeuagiza Uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora kuanza kuwakata fedha katika mishahara yao watumishi wote wanaodaiwa masurufu ya safari ambao wameshindwa kufanya marejesho kwa muda mrefu na hivyo kusababisha kupata hati yenye mashaka.
Kauli hiyo imetolewa leo katika Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Tabora ambao ulikuwa ikipitia taarifa mbalimbali ikiwemo ya Mkaguzi wa Ndani wa Hesabu. Diwani wa Kata ya Ndevelwa Selemani Maganga alisema haiwezekani Halmashauri hiyo iendelee kupata hoja inayotokana na watumishi kushindwa kufanya marejesho ya fedha walizopewa kwa ajili ya safari ya kikazi.
Alitaka watumishi wote wanaodaiwa waanze kukatwa katika mshahara wao wa Mwezi ujao(Septemba) ili fedha hizo zirejeshwe katika Halmashauri hiyo kwa ajili ya shughuli nyingine. Naye Diwani wa Kata ya Kanyenye na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoani Tabora .Ghulam Dewji alisema urejeshaji wa masurufu ya safari kwa watumishi wa Manispaa ya Tabora hauridhishi na kutaka hatua kali dhidi yao zichukuliwe.
Alisema miongoni mwa hoja zilizosababishia kupata hati yenye mashaka iliyotokana na ukaguzi uliofanywa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ni masurufu yanafikia shilingi milioni 84 ambazo watumishi hawajafanya marejesho. Dewji alisema kati ya fedha hizo ni milioni 11 ndio zimefanyiwa marejesho kwa mujibu wa Mkaguzi wa Ndani wa Hesabu wa Manispaa ya Tabora , bado milioni 73 hazijafanyiwa marejesho.
Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Tabora Bosco Nduguru akitoa ufafanuni kwa Madiwani leo juu hatua ambazo wameanza kuzichukua katika kuhakikisha wanafuta hoja ya masurufu yenye thamani ya milioni 84 ambayo hajafanyiwa marejesho na watumishi wa Halmashauri hiyo.
Hivyo makala WADAIWA WA MASURUFU YA SAFARI KATIKA MANISPAA YA KUKATWA KATIKA MISHAHARA YAO YA SEPTEMBA
yaani makala yote WADAIWA WA MASURUFU YA SAFARI KATIKA MANISPAA YA KUKATWA KATIKA MISHAHARA YAO YA SEPTEMBA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WADAIWA WA MASURUFU YA SAFARI KATIKA MANISPAA YA KUKATWA KATIKA MISHAHARA YAO YA SEPTEMBA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/wadaiwa-wa-masurufu-ya-safari-katika.html
0 Response to "WADAIWA WA MASURUFU YA SAFARI KATIKA MANISPAA YA KUKATWA KATIKA MISHAHARA YAO YA SEPTEMBA"
Post a Comment