title : Maafisa Habari Watekeleze Wajibu Wa Kutoa Habari kwa Umma
kiungo : Maafisa Habari Watekeleze Wajibu Wa Kutoa Habari kwa Umma
Maafisa Habari Watekeleze Wajibu Wa Kutoa Habari kwa Umma
Na Grace Semfuko-MAELEZO
Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi amewataka Maafisa Habari Nchini kufanya kazi zao kwa kufuata sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 ambayo inawapa fursa Waandishi wa Habari kupata,kuhariri na kurusha habari kwa wananchi ili waweze kuelewa maendeleo ya nchi yao.
Ameyasema hayo wakati akizungumza kwa nyakati tofauti Jijini Dar Es Salaam Ijumaa Agosti 24, 2018 alipotembelea Kampuni ya Magazeti ya New Habari na Shirika la Habari linalounganisha Redio zenye Maudhui ya kijamii la TADIO ambao walimweleza Msemaji Mkuu wa Serikali kuhusiana na changamoto za kupata habari wanazofanyiwa na baadhi ya Maafisa Habari wa Taasisi mbalimbali za Serikali Nchini.
“Ni kweli wapo baadhi ya Maafisa Habari ambao wanakwamisha juhudi za waandishi kupata Habari,Idara ya Habari MAELEZO tumeliona hilo na tulishaanza mkakati wa kuhakikisha kila taasisi inatoa habari ili wananchi waelewe maendeleo ya maeneo yao na taasisi hizo, tumekaa na Maafisa Habari mara kadhaa na tumewapa mafunzo na sasa changamoto hiyo imepungua kwa kiasi kikubwa” alisema Dkt Abbasi.
Sheria hiyo iliyopitishwa na Bunge Novemba 5 Mwaka 2016 na Kusainiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Novemba 16 mwaka huo huo wa 2016, pamoja na mambo mengine, inalenga kulinda maslahi ya waandishi wa habari,kulinda kazi zao pamoja na kuboresha Taaluma hiyo ili iweze kuheshimika kama taaluma ilivyo kwa zingine.
Aidha Dkt. Abbasi amezungumzia mkakati wa kuanzishwa kwa mfuko wa taaluma ya habari ili kuwawezesha waandishi kumudu kufanya kazi za utafiti wa habari na vipindi mbalimbali vya kijamii badala ya kutegemea ruzuku za mashirika ambazo pia huja kwa masharti ambayo mengi yanaweza kuwaingiza hatiani.
Aidha Dkt. Abbasi pia amewakumbusha Waandishi wa Habari nchini kujiunga na vyuo mbalimbali ili kujiendeleza kitaaluma na hatimaye waweze kuendana na kanuni ya kuwa na diploma itakayoanza kutumika mwishoni mwa mwaka 2021.
“Kanuni ya kumtaka mwanahabari awe na diploma kwenda juu katika fani ya habari itaanza kutumika mwaka 2021, tumetoa muda wa kutosha kabisa kwa waandishi kujiendeleza,kama hukufanya hivyo sheria haitakuruhusu kupata ithibati ya kuendelea na majukumu ya kazi za Habari,” alisisitiza Dkt. Abbasi.

Hivyo makala Maafisa Habari Watekeleze Wajibu Wa Kutoa Habari kwa Umma
yaani makala yote Maafisa Habari Watekeleze Wajibu Wa Kutoa Habari kwa Umma Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Maafisa Habari Watekeleze Wajibu Wa Kutoa Habari kwa Umma mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/maafisa-habari-watekeleze-wajibu-wa.html
0 Response to "Maafisa Habari Watekeleze Wajibu Wa Kutoa Habari kwa Umma"
Post a Comment