VICHAKA VYA ITIGI ‘ITIGI THICKETS’ HATARINI KUTOWEKA

VICHAKA VYA ITIGI ‘ITIGI THICKETS’ HATARINI KUTOWEKA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa VICHAKA VYA ITIGI ‘ITIGI THICKETS’ HATARINI KUTOWEKA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : VICHAKA VYA ITIGI ‘ITIGI THICKETS’ HATARINI KUTOWEKA
kiungo : VICHAKA VYA ITIGI ‘ITIGI THICKETS’ HATARINI KUTOWEKA

soma pia


VICHAKA VYA ITIGI ‘ITIGI THICKETS’ HATARINI KUTOWEKA

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mheshimiwa January Makamba hii leo amehitimisha ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Singida na kuwasili katika Mkoa wa Tabora, ikiwa ni mwendelezo wa kukagua, kutathmini, kuzungumza na viongozi, na wananchi kuhusu maeneo yanayopendekezwa kuhifadhiwa kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira, sambamba na uanzishwaji na ufuatiliaji utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi Mazingira ya mwaka 2004 katika ngazi za Serikali za Mitaa. 

Katika siku ya tatu ya ziara yake Mhe. Makamba ametembelea vichaka vya Itigi ‘Itigi thicket” na kupata fursa ya kuzungumza na viongozi wa wilaya ya Manyoni juu ya namna bora ya kuhifadhi eneo hilo lenye ukubwa wa hekta 410,000 na kuahidi kutuma wataalamu kuandaa andiko la Mradi utakaonufaisha wakazi wa eneo hilo katika sekta uvunaji wa asali kwa njia ya kisasa zaidi.

“Ndani ya muda mfupi nitatuma wataalamu wangu kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC, waje wakae na wataalamu wenu na kuandaa Mradi utaonufaisha wakazi wa wanaozunguka eneo lote la msitu ili kutunza na kuhifadhi rasilimali za asili zilizopo katika eneo hili” Makamba alisisitiza.

Katika hatua nyingine Waziri Makamba amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Bi. Rahabu Jackson kuwasilisha kwake majina wa watalaamu wa Mazingira ambao wana sifa za kuwa Wakaguzi wa Mazingira ili waweze kuteuliwa kwa mujibu wa Sheria.
Mwananchi ambae jina lake halikupatikana mara moja amejikita katika suala la hifadhi ya vichaka vya Itigi, ambavyo humsaidia kuongeza kipato kwa kuvuna asali. 
Sehemu ya vichaka adimu duniani vinavyopatikana Itigi, “Itigi thickets” katika bara la Afrika vichaka kama hivyo vinapatikana Tanzania na Zambia pekee, viko hatarini kutoweka kutoweka kutokana na shughuli za kibinadamu. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akisalimiana na Bw. Khatib Ally mmoja wa wananchi waliojitokeza kumpokea katika Kijiji cha Aghondi Wilayani Manyoni, Mkoani Singida. Waziri Makamba ametembelea eneo hilo ambalo lina vichaka vya aina yake na vyakipekee barani Afrika. Wananchi wa eneo hilo wamewasilisha ombi kwa Waziri Makamba la kuweka ulinzi wa kutosha na namna bora ya kuhifadhi eneo hilo. 

 



Hivyo makala VICHAKA VYA ITIGI ‘ITIGI THICKETS’ HATARINI KUTOWEKA

yaani makala yote VICHAKA VYA ITIGI ‘ITIGI THICKETS’ HATARINI KUTOWEKA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala VICHAKA VYA ITIGI ‘ITIGI THICKETS’ HATARINI KUTOWEKA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/vichaka-vya-itigi-itigi-thickets.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "VICHAKA VYA ITIGI ‘ITIGI THICKETS’ HATARINI KUTOWEKA"

Post a Comment