TRA YAENDELEA KUTOA ELIMU YA MSAMAHA WA RIBA NA ADHABU YA MALIMBIKIZO YA KODI

TRA YAENDELEA KUTOA ELIMU YA MSAMAHA WA RIBA NA ADHABU YA MALIMBIKIZO YA KODI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TRA YAENDELEA KUTOA ELIMU YA MSAMAHA WA RIBA NA ADHABU YA MALIMBIKIZO YA KODI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TRA YAENDELEA KUTOA ELIMU YA MSAMAHA WA RIBA NA ADHABU YA MALIMBIKIZO YA KODI
kiungo : TRA YAENDELEA KUTOA ELIMU YA MSAMAHA WA RIBA NA ADHABU YA MALIMBIKIZO YA KODI

soma pia


TRA YAENDELEA KUTOA ELIMU YA MSAMAHA WA RIBA NA ADHABU YA MALIMBIKIZO YA KODI

Na Veronica Kazimoto-Kigoma

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inaendelea kutoa elimu juu ya namna ya kuomba msamaha wa riba na adhabu ya malimbikizo ya madeni ya kodi kwa wafanyabiashara na wadau mbalimbali nchini.

Akizungumza wakati wa semina elekezi kwa wafanyabiashara na wadau mbalimbali mkoani Kigoma, Afisa Elimu Mkuu kwa Mlipakodi wa mamlaka hiyo Rose Mahendeka amewaambia wafanyabiashara hao kuwa lengo la kutoa msamaha huo ni kuwapunguzia mzigo ili waweze kulipa kodi ya msingi isiyokuwa na riba wala adhabu ambapo mwisho wa kulipa kodi hiyo ni tarehe 30 Juni, 2019.

“Serikali imeamua kutoa msamaha wa riba na adhabu kwenye malimbikizo ya madeni ya kodi kwa asilimia 100 ili kuwasaidia wafanyabiashara kulipa kodi ya msingi tu ambayo mfanyabiashara anaweza kuilipa mara moja au kwa awamu ndani ya Mwaka wa Fedha 2018/19,” alisema Mahendeka.

Mahendeka ameeleza kuwa, msamaha huu ni wa miezi 6 na ulianza mwezi Julai na utamalizika Desemba, 2018 na kuongeza kuwa huu ni muda muafaka wa wafanyabiashara hao kutuma maombi ya msamaha huo kabla muda uliopangwa haujamalizika.

“Natumia fursa hii kuwasihi wafanyabiashara kutuma maombi TRA ya msamaha huu kabla ya mwezi Novemba, 2018 na msisite kuwasiliana na ofisi yetu ya hapa mkoani pindi mtakapohitaji ufafanuzi zaidi,” aliongeza Mahendeka.Aidha, Mahendeka alisisitiza kuwa TRA itatoa majibu ya maombi ya msamaha huo kwa maandishi ndani ya siku thelathini (30) tangu siku ya kupokea maombi.
Afisa Elimu Mkuu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Rose Mahendeka akitoa elimu juu ya msamaha wa riba na adhabu ya malimbikizo ya madeni ya kodi wakati wa semina elekezi kwa wafanyabiashara na wadau mbalimbali iliyofanyika mkoani Kigoma kwa lengo la kutoa uelewa kuhusu msamaha huo.

Afisa Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Chama Siriwa akiwasilisha mada kuhusu msamaha wa riba na adhabu ya malimbikizo ya madeni ya kodi wakati wa semina elekezi kwa wafanyabiashara na wadau mbalimbali iliyofanyika mkoani Kigoma kwa lengo la kutoa uelewa kuhusu msamaha huo.

Baadhi ya wafanyabiashara na wadau mbalimbali waliohudhuria semina elekezi ya msamaha wa riba na adhabu ya malimbikizo ya madeni ya kodi iliyofanyika mkoani Kigoma kwa lengo la kutoa uelewa kuhusu msamaha huo.

Baadhi ya wafanyabiashara na wadau mbalimbali waliohudhuria semina elekezi ya msamaha wa riba na adhabu ya malimbikizo ya madeni ya kodi iliyofanyika mkoani Kigoma kwa lengo la kutoa uelewa kuhusu msamaha huo. 




Hivyo makala TRA YAENDELEA KUTOA ELIMU YA MSAMAHA WA RIBA NA ADHABU YA MALIMBIKIZO YA KODI

yaani makala yote TRA YAENDELEA KUTOA ELIMU YA MSAMAHA WA RIBA NA ADHABU YA MALIMBIKIZO YA KODI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TRA YAENDELEA KUTOA ELIMU YA MSAMAHA WA RIBA NA ADHABU YA MALIMBIKIZO YA KODI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/tra-yaendelea-kutoa-elimu-ya-msamaha-wa_26.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TRA YAENDELEA KUTOA ELIMU YA MSAMAHA WA RIBA NA ADHABU YA MALIMBIKIZO YA KODI"

Post a Comment