Taasisi ya fahari ya Tuamke yawataka wananchi kusaidia Jamii

Taasisi ya fahari ya Tuamke yawataka wananchi kusaidia Jamii - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Taasisi ya fahari ya Tuamke yawataka wananchi kusaidia Jamii, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Taasisi ya fahari ya Tuamke yawataka wananchi kusaidia Jamii
kiungo : Taasisi ya fahari ya Tuamke yawataka wananchi kusaidia Jamii

soma pia


Taasisi ya fahari ya Tuamke yawataka wananchi kusaidia Jamii




Diwani wa Kata ya Pugu Stesheni Yohana Ng'ong'a akikabidhi daftari na Michele kwa Mwanafunzi wa darasa la sita shule ya msingi Bangulo vilivyotolewa na Taasisi ya Fahari Tuamke Maendeleo kwa ajili ya kusaidia shule hiyo, jumla ya wanafunzi 100 wa mazingira magumu walipata msaada, (Kushoto MWALIMU Mkuu wa Shule hiyo Wilfredy Luyagaza na MWENYEKITI wa Taasisi ya Fahari Neema Mchau.

Mwenyekiti wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Fahari Tuamke Maendeleo Neema Chau akizunngumza wakati taasisi hiyo ilipokwenda kutoa msada katika Shule ya MSINGI Bangulo Pugu Stesheni Wilayani Ilala (Picha na Heri Shaban)

Na Heri Shaban
Mwambawahabari
TAASISI ya fahari Tuamke Maendeleo iliyopo Wilayani Ilala imewataka wananchi kujitolea kusaidia Jamii  inayowazunguka ambao Wapo katika mazingira magumu.

Hayo yalisemwa Dar es salaam Leo na na mratibu wa Kituo cha Fahari Tuamke Maendeleo Tausi Mfaume wakati wa kutoa msaada wa Vifaa vya shule na Chakula kwa baadhi ya wanafunzi wa Shule ya MSINGI Dangulo iliyopo Pugu Stesheni Dar es salaam.

Tausi alisema wananchi wenye kipato inatakiwa kujenga tabia ya kusaidia wa wenye mazingira magumu wakiwemo wanafunzi ili waweze kupata elimu.

"Taasisi yetu siyo ya kiserikali ya Fahari Tuamke MAENDELEO inashughulika pia kusaidia makundi mbalimbali ya Vijana walio katika mazingira magumu sambamba na Wanafunzi waliopo shule ambao Wazazi wao hawana uwezo  kwa kuwasaidia vifaa vya shule,"alisema Tausi.

Tausi alisema taasisi yao ya kituo cha kulea watoto wadogo ilianzishwa mwaka 2016  imekuwa ikijishughulisha na shughuli zake pamoja na kuisaidia Serikali katika kuunga mkono sekta ya elimu bure kwa kutoa vifaa vya shule kwa baadhi ya shule pamoja na kutoa misaada kwa makundi ya walemavu na Yatima.

Aidha alisema kabla kutoa msaada huo awali walishirikiana na Ofisa Maendeleo ya Kata ambapo aliwachagulia shule hiyo ambapo walitoa vifaa vya shule, Chakula na wanafunzi nane wa Shule Dangulo watawagharamia kuwalipia gharama zote za pre form one couse kwa ajili ya maandalizi ya sekondari kutokana na WAZAZI wao kukosa uwezo kifedha.


Kwa upande wa Mwenyekiti wa Fahari Tuamke MAENDELEO Neema Chau, alisema taasisi hiyo inashirikiana na Serikali umeamua kuwekeza katika elimu ili kusaidia watoto wa Wazazi wenye mazingira magumu waweze kupata elimu.

Neema alisema watoto wote wana haki ya kupata elimu na taasisi hiyo imekuwa ikijitolea kusaidia baadhi ya watoto ambao wanasoma katika Shule za Serikali ambazo zipo Jirani na taasisi hiyo.

Alisema taasisi hiyo ni changa mbali na Uchanga wake lakini imekuwa ikiwajibika kutekeleza malengo yake ambayo ni pamoja na kuwatambua watoto ambao wanaishi mazingira magumu na kuwapatia mahitaji ya msingi.

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo ya Bangulo Wilfred Luyagaza alisema shule hiyo ilianzishwa mwaka 2002 ina idadi ya walimu 26 na Wanafunzi 2384.

Mwisho


Hivyo makala Taasisi ya fahari ya Tuamke yawataka wananchi kusaidia Jamii

yaani makala yote Taasisi ya fahari ya Tuamke yawataka wananchi kusaidia Jamii Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Taasisi ya fahari ya Tuamke yawataka wananchi kusaidia Jamii mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/taasisi-ya-fahari-ya-tuamke-yawataka.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Taasisi ya fahari ya Tuamke yawataka wananchi kusaidia Jamii"

Post a Comment