SINGIDA WAASWA KUACHA MILA POTOFU

SINGIDA WAASWA KUACHA MILA POTOFU - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SINGIDA WAASWA KUACHA MILA POTOFU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SINGIDA WAASWA KUACHA MILA POTOFU
kiungo : SINGIDA WAASWA KUACHA MILA POTOFU

soma pia


SINGIDA WAASWA KUACHA MILA POTOFU

Wakazi wa Mkoa wa Singida wanaoendeleza mila potofu ya ukeketaji, wameaswa kuachana na mila hiyo, badala yake waanzishe vilabu kwa lengo la kuwafundisha wasichana umuhimu wa kufanya kazi halali na maadili mema kupunguza kasi ya mmomonyoko wa maadili.
 Mwito huo ulitolewa na Dk Getrude Mughamba kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Singida wakati wa warsha iliyohudhuriwa na vikundi kazi na watendaji wa kata, wanaoshiriki utekelezaji wa mradi wa kutokomeza vitendo vya ukeketaji.
Mradi huo unaotekelezwa katika kata nne za halmashauri hiyo, unaendeshwa na Shirika la Empower Society to Transform Lives (ESTL) kwa ufadhili wa Shirika la Foundation for Civil Society. Dk Mughamba alieleza kuwa kupitia vilabu hivyo, wasichana watapata fursa ya kufundishwa mapishi bora, usafi na utunzaji wa mazingira na namna bora ya kuishi na mume; hivyo kurejesha nidhamu na maadili mema ya namna ya kuishi katika jamii iliyostaarabika.
Alisema kuwa jamii ya kabila la Wanyaturu na makabila mengine yanayoendelea kukumbatia mila hiyo potofu ya ukeketaji ambao wamekuwa wakifanya hivyo kwa ajili ya kujipatia sifa ya kuolewa hivi sasa hawana budi kubadili mfumo wa mila na utamaduni wenye tija. Alisema kuwa kwa kuanzisha vilabu vya aina hiyo, jamii itawafunda watoto wao kwa namna bora zaidi, badala ya kuendelea kuwakeketa hali inayowatia kwenye machungu ya kujifungua kwa taabu, kutofurahia vyema tendo la ndoa na kuwaathiri milele kisaikolojia.


Hivyo makala SINGIDA WAASWA KUACHA MILA POTOFU

yaani makala yote SINGIDA WAASWA KUACHA MILA POTOFU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SINGIDA WAASWA KUACHA MILA POTOFU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/singida-waaswa-kuacha-mila-potofu.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SINGIDA WAASWA KUACHA MILA POTOFU"

Post a Comment