title : SERIKALI KUBORESHA KISIWA CHA MAGAFU KATIKA ZIWA VICTORIA WILAYANI CHATO MKOA WA GEITA
kiungo : SERIKALI KUBORESHA KISIWA CHA MAGAFU KATIKA ZIWA VICTORIA WILAYANI CHATO MKOA WA GEITA
SERIKALI KUBORESHA KISIWA CHA MAGAFU KATIKA ZIWA VICTORIA WILAYANI CHATO MKOA WA GEITA
Na Richard Bagolele, Chato
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano) January Makamba amesema serikali inaangalia uwezekano wa kilinda na kukihifadhi kisiwa cha Magafu kilichopo Wilayani Hapa ili kiwe kivutio cha Utalii na eneo maalumu kwa ajili ya mazalia ya Samaki.
Waziri Makamba amesema hayo alipotembelea kisiwa hicho kufuatia ombi la Halmashauri ya Wilaya ya Chato kwa Wizara hiyo la kuomba kisiwa hicho kihifadhiwe na kuwa eneo lindwa kuwa eneo tengefu kwa ajili ya mazalia ya samaki kwa ziwa Viktoria.
‘’kutokana eneo la kisiwa hiki kuwa ni chanzo kikubwa cha mazalia ya samaki lakini kumekuwa na hatari kubwa za uvamizi wa kisiwa hiki kutokana na shughuli za kilimo, uvuvi haramu na ufugaji ambao umeathiri ukuaji wa samaki na shughuli nzima za kiuchumi” alisema Waziri Makamba.
Amesema kutokana na umuhimu wa kisiwa hicho, Wizara yake itaandaa mpango wa matumizi mazuri ya kisiwa hicho ili kiweze kurudi kwenye mazingira yake ya asilia kwa kushirikiana na uongozi wa Wilaya ya Chato na Jamii inayozunguka eneo hilo.
Kwa upande Mkuu Wa Wilaya ya Chato Mhandisi Mtemi Msafiri amesema kutokana na umuhimu wa kisiwa hicho kiuchumi ni lazima kisiwa hicho kihifadhiwe ili kuongeza samaki ziwa viktoria na shughuli za kiutalii kwani mahali hapo panaweza kujengwa hoteli ya kitalii kwani kisiwa hicho kipo karibu na hifadhi ya kisiwa cha Rubondo.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri Christian Manunga ameomba kisiwa hicho kianze kulindwa ili kunusuru maliasili zilizomo kwa manuaa ya serikali hususan Wilaya ya Chato.
Kisiwa kidogo cha Magafu kipo ndani ya Ziwa Viktoria eneo la kata ya Nyamirembe. Kisiwa hicho kinakadiriwa kuwa na ukubwa eneo wa mita 3 za mraba.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano) January Makamba akiwa ameongozana na viongozi wa Wilaya ya Chato wakiangalia mazingira ya kisiwa Cha Magafu kilichopo kata ya Nyamirembe wilayani Chato.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano) January Makamba akiangalia mazingira ya kisiwa Cha Magafu kilichopo kata ya Nyamirembe wilayani Chato.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano) January Makamba pamoja na viongozi wengine wakiwa kwenye lango la kuingilia kisiwa cha Magafu kilichopo kata ya Nyamirembe wilayani Chato.
Hivyo makala SERIKALI KUBORESHA KISIWA CHA MAGAFU KATIKA ZIWA VICTORIA WILAYANI CHATO MKOA WA GEITA
yaani makala yote SERIKALI KUBORESHA KISIWA CHA MAGAFU KATIKA ZIWA VICTORIA WILAYANI CHATO MKOA WA GEITA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI KUBORESHA KISIWA CHA MAGAFU KATIKA ZIWA VICTORIA WILAYANI CHATO MKOA WA GEITA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/serikali-kuboresha-kisiwa-cha-magafu.html
0 Response to "SERIKALI KUBORESHA KISIWA CHA MAGAFU KATIKA ZIWA VICTORIA WILAYANI CHATO MKOA WA GEITA"
Post a Comment