PREMIER BET YAZINDUA RASMI FOOTBALL JACKPOT

PREMIER BET YAZINDUA RASMI FOOTBALL JACKPOT - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa PREMIER BET YAZINDUA RASMI FOOTBALL JACKPOT, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : PREMIER BET YAZINDUA RASMI FOOTBALL JACKPOT
kiungo : PREMIER BET YAZINDUA RASMI FOOTBALL JACKPOT

soma pia


PREMIER BET YAZINDUA RASMI FOOTBALL JACKPOT

Mkurugenzi Mtendaji wa Premier Bet, Samir Matar (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Football Jackpot   utakaowapa fursa wateja wa kampuni hiyo kujinyakulia kitita kikubwa cha fedha cha Shillingi Milioni 15.5 za Kitanzania.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.


Kampuni ya Michezo ya Kubashiri ya Premier Bet imezindua mchezo mpya wa Football Jackpot utakaowapa fursa wateja wa kampuni hiyo kujinyakulia kitita kikubwa cha fedha cha Shillingi Milioni 15.5 za Kitanzania.

Jackpot hiyo iliyozinduliwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Premier Bet, Samir Matar utakuwa mchezo wa kwanza wa Jackpot wenye kima kidogo katika michezo ya kubashiri nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari, Matar amesema kuwa Jackpot hiyo itakayohusisha mechi 12 za ligi mbalimbali droo yake itakuwa inachezwa kila siku ya Jumatano saa 3.55 usiku na Jumamosi saa 10.55 jioni.

Ameeleza kuwa, wateja watatakiwa kubashiri mechi 12 zitakazokuwa zimeorodheshwa kwa mawakala wote nchini na atafanikiwa kushinda kitita hicho cha Milioni 15.5 na ikitokea mteja akabashiri mechi 10 au 11 atapatiwa fedha kulingana na ubashiri wake.

Meneja Rasilimali watu na Utawala Amanda Kombe amesema kuwa lengo la kuanzisha Jackpot hii ni kwa ajili ya kukuza burudani ya soka kwa wateja wa Premier Football Betting ili kuwapa fursa ya kushinda kitita kikubwa cha fedha kwa kutoa hela kidogo.

Amanda amesema, kama ikitokea katika siku ambayo Jackpot imechezeshwa mshinda wa Milioni 15 hajapatikana hivyo inapelekea kuongezeka kwa kiwango cha fedha.

Kwa sasa Premier Bet ina jumla ya mawakala 2000 nchini kote na ratiba za mechi zitakazokuwa zinashindanishwa zitakuwa zinapatikana kwa mawakala hao na mteja anaweza kucheza kadri ya uwezo wake. 

Meneja Rasilimali watu na Utawala Amanda Kombe akiwaonyesha waandishi wa Habari aina ya tiketi ya michezo ya kubashiri ya Premier Bet wakati wa uzinduzi wa Jackpot ya Premier Bet Jijini Dar es Salaam.


Wafanyakazi wa Premier Bet wakionyesha namna ya kutoa risiti katika mashine kwa Mkurugenzi Mtendaji Samir Matar ( picha ya juu)  pia wakitoa tiketi kwa waandishi wa habari waliofika katika uzinduzi huo.


Hivyo makala PREMIER BET YAZINDUA RASMI FOOTBALL JACKPOT

yaani makala yote PREMIER BET YAZINDUA RASMI FOOTBALL JACKPOT Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala PREMIER BET YAZINDUA RASMI FOOTBALL JACKPOT mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/premier-bet-yazindua-rasmi-football.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "PREMIER BET YAZINDUA RASMI FOOTBALL JACKPOT"

Post a Comment