title : NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA UCHUKUZI AAGIZI WAFANYAKAZI WALIOJIGAWIA VIWANJA WANYANG'ANYWE
kiungo : NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA UCHUKUZI AAGIZI WAFANYAKAZI WALIOJIGAWIA VIWANJA WANYANG'ANYWE
NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA UCHUKUZI AAGIZI WAFANYAKAZI WALIOJIGAWIA VIWANJA WANYANG'ANYWE
Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii
NAIBU Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Atashasta Nditiye, ameagiza wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) ambao walijigawia viwanja katika viwanja vya fidia za wananchi wanyang'anywe na kufikishwa mahakamani ili sheria ifuate mkondo wake.
Ameyasema hayo wakati alipofanya kikao na wawakilishi wa mkuu wa mkoa pamoja na wawakilishi wa kampuni ya Tanzania Remic centre jijini Dar es Salaam leo Agosti 30,2018.ambapo alieleza wasiwasi wake kuwa kampuni iliyopewa kandarasi ya kuwatafutia viwanja wananchi hao haijatekeleza wajibu wake ipasavyo licha ya kuwa tayari imelipwa kiasi cha shilingi bilioni 3.7.
Nditiye pia ameagiza Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, wakakague viwanja 537 vilivyotengwa maeneo ya Msongola, kwa ajili ya waliokuwa wakazi wa eneo la Kipawa jijini Dar es Salaam Jumanne wiki ijayo ili kujiridhisha kama viwanja hivyo vipo na vinafaa.
“Nakuagiza Mkurugenzi wa TAA, kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Wilaya Jumanne ijayo muende mkakague eno hilo la viwanja 537 muone kama vipo kwa sababu kumekuwa na shida sana na hawa wenzetu wa Tanzania Remix Centre nyinyi wenyewe mnajua, kuna shida ya miundombinu, sasa lazime mjue eneo hilo linafikika, na viwanja hivyo vinajengeka.” Amesema.
Amesema Wananchi wako tayari kushirikiana na serikali katika kuhakikisha upanuzi wa uwanja unakwenda vizuri. Kampuni ya Tanzania Remix Centre ilipendekezwa na Manispaa ya Ilala na kupewa kandarasi ya kutafuta viwanja kwa ajili ya makazi mapya ya wananchi waliokuwa wakiishi eneo la Kipawa jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo kulikuwepo na mivutano kati ya Mamlaka na Wananchi ambapo baadhi yao walipeleka shauri hilo mahakamani na hivyo kufanya zoezi hilo la kuwahamisha wananchi hao kwenye eneo hilo jipya kusuasua.
“Mradi huu ulihusisha upatikanaji wa viwanja 1,600 kwa mujibu wa mkataba wa awali ambapo fidia yake ilipaswa kufanywa kwa awamu mbili ya watu 800, hata hivyo kwa mujibu wa sheria kipinde kile ilitaka mwananchi apewe eneo lakini alipwe fidia pia.” Amefafanua.
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Atashasta Nditiye akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kikao kati ya wawakilishi wa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam na Kampuni ya Tanzania Remix Centre katika ukumbi wa VIP terminal II uliopo Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere.
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Atashasta Nditiye akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA),Richard Mayongela.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA),Richard Mayongela akizungmza wakati wa kikao na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Atashasta Nditiye kulia leo jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa kampuni ya Tanzania Remix centre akizungumza wakati wa kikao kilichofanyika leo katika ukumbi wa VIP terminal II uliopo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere kulia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Atashasta Nditiye.
Hivyo makala NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA UCHUKUZI AAGIZI WAFANYAKAZI WALIOJIGAWIA VIWANJA WANYANG'ANYWE
yaani makala yote NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA UCHUKUZI AAGIZI WAFANYAKAZI WALIOJIGAWIA VIWANJA WANYANG'ANYWE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA UCHUKUZI AAGIZI WAFANYAKAZI WALIOJIGAWIA VIWANJA WANYANG'ANYWE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/naibu-waziri-wa-mawasiliano-na-uchukuzi.html
0 Response to "NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA UCHUKUZI AAGIZI WAFANYAKAZI WALIOJIGAWIA VIWANJA WANYANG'ANYWE"
Post a Comment