ALAT TABORA YAIPONGEZA UYUI KWA MATUMIZI MAZURI KWENYE UJENZI WA VYUMBA VYA SHULE YA LOLANGULU

ALAT TABORA YAIPONGEZA UYUI KWA MATUMIZI MAZURI KWENYE UJENZI WA VYUMBA VYA SHULE YA LOLANGULU - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa ALAT TABORA YAIPONGEZA UYUI KWA MATUMIZI MAZURI KWENYE UJENZI WA VYUMBA VYA SHULE YA LOLANGULU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : ALAT TABORA YAIPONGEZA UYUI KWA MATUMIZI MAZURI KWENYE UJENZI WA VYUMBA VYA SHULE YA LOLANGULU
kiungo : ALAT TABORA YAIPONGEZA UYUI KWA MATUMIZI MAZURI KWENYE UJENZI WA VYUMBA VYA SHULE YA LOLANGULU

soma pia


ALAT TABORA YAIPONGEZA UYUI KWA MATUMIZI MAZURI KWENYE UJENZI WA VYUMBA VYA SHULE YA LOLANGULU


NA TIGANYA VINCENT-TABORA

Jumuiya ya Serikali za mitaa Tanzania ( ALAT) Mkoani Tabora imeipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Tabora -Uyui kufanikisha ukamishaji wa ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika Shule ya Msingi Lolangulu kwa kiasi cha shilingi milioni 38.

Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Tabora Adam Malunkwi wakati wajumbe wa Jumuiya hiyo wakiwa katika kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo kwa ajili ya kubadilishana uzoefu.

Alisema juhudi za Kamati ya Shule hiyo kwa kushirikiana na wananchi zimewapa fundisho kuwa miradi mingi inaweza kutekelezwa kwa fedha kidogo na kwa ubora wa hali ya juu. Mbunge wa Jimbo la Manonga Seif Gulamali alisema Vyumba vipya vya madarasa katika Shule hiyo vinapaswa kutumika kama funzo kwa watu wanaosimamia miradi ya ujenzi katika Mkoa wa Tabora.

Alisema hali hiyo imeonyesha kuwa wakipewa na Serikali shilingi milioni 64 wanaweza kujenga vyumba zaidi ya vinne vikiwa vimekamilika na samani zake kama walivyoona katika Shule ya Lolangulu. Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega Kiwele Bundala alimwagiza Mkurugenzi Mtendaji wake kuhakikisha anatuma wataalamu wake wa ujenzi ili waweze kujifunza mbinu walizotumia wakazi wa pale na Kamati yao kufanikisha mradi huo kwa kiwango cha juu.

Alisema hatua ya wao kuweza kujenga vyumba vitatu vikiwa na samani kwa fedha hizo kimeonyesha jinsi miradi mingi ya maendeleo ya wananchi inaweza kufanyika kwa kiwango kidogo cha fedha. Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Margaret Nakainga alisema wataalamu wa ujenzi katika Halmashauri za Mkoa wa Tabora watakiwa waige mfano wa ujenzi wa vyumba vingi vya madarasa kama vya shule ya Lolangulu ambapo vimewekewa na makinga maji.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Lolangulu Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora Mary Zacharia akisoma taarifa jana ya ujenzi wa mradi wa vyumba vitatu vya madarasa na uwekaji wa samani kwa gharama ya milioni 38 kwa wajumbe 
Jengo lenye vyumba vitatu vya madarasa na samani zake lilipo katika Shule ya Msingi Lolalungu wilayani Uyui Mkoani Tabora ambalo limegharimu milioni 38 hadi kukamilika. 
Wajumbe wa Jumuiya ya Serikali za mitaa Tanzania ( ALAT) Mkoani Tabora wakikagua na kupata taarifa jana ya mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa matatu katika Halmashauri ya Wilaya ya Tabora -Uyui kwenye Shule ya Msingi Lolangulu vilivyogharimu milioni 38. 



Hivyo makala ALAT TABORA YAIPONGEZA UYUI KWA MATUMIZI MAZURI KWENYE UJENZI WA VYUMBA VYA SHULE YA LOLANGULU

yaani makala yote ALAT TABORA YAIPONGEZA UYUI KWA MATUMIZI MAZURI KWENYE UJENZI WA VYUMBA VYA SHULE YA LOLANGULU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala ALAT TABORA YAIPONGEZA UYUI KWA MATUMIZI MAZURI KWENYE UJENZI WA VYUMBA VYA SHULE YA LOLANGULU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/alat-tabora-yaipongeza-uyui-kwa_30.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "ALAT TABORA YAIPONGEZA UYUI KWA MATUMIZI MAZURI KWENYE UJENZI WA VYUMBA VYA SHULE YA LOLANGULU"

Post a Comment