MUHAS YATANGAZA KIFO CHA MAREHEMU PROFESA EMIL N. KIKWILU

MUHAS YATANGAZA KIFO CHA MAREHEMU PROFESA EMIL N. KIKWILU - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MUHAS YATANGAZA KIFO CHA MAREHEMU PROFESA EMIL N. KIKWILU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MUHAS YATANGAZA KIFO CHA MAREHEMU PROFESA EMIL N. KIKWILU
kiungo : MUHAS YATANGAZA KIFO CHA MAREHEMU PROFESA EMIL N. KIKWILU

soma pia


MUHAS YATANGAZA KIFO CHA MAREHEMU PROFESA EMIL N. KIKWILU

MAKAMU Mkuu wa Chuo anasikitika kutangaza kifo cha Profesa Emil Namakuka Kikwilu kilichotokea usiku wa tarehe 27/08/2018 maeneo ya Kimara, Dar es Salaam.

Prof. Kikwilu ametumikia Chuo katika nyadhifa mbalimbali kama Mkuu wa Skuli ya Afya ya Kinywa na Meno mwaka 1991 – 1997 na mwaka 2006 – 2009 na pia kama Naibu Mrajisi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Sayansi za Afya Muhimbili mwaka 2002 - 2003. Kabla ya kifo chake marehemu Emil N. Kikwilu alikuwa Profesa katika Idara ya Afya ya Kinywa na Meno kwa Watoto na Jamii (Department of Orthodontics, Paedodontics and Community Dentistry) katika Skuli ya Afya ya Kinywa na Meno.

Mwili wa marehemu Prof. Kikwilu utaagwa na wanajumuia wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi siku ya Alhamisi tarehe 29 Agosti 2018, kuanzia saa nane kamili mchana katika eneo la Chuo kampasi ya Muhimbili. Marehemu anatarajiwa kuzikwa siku ya Ijumaa tarehe 31 Agosti 2018, Kimara mwisho.

Makamu Mkuu wa Chuo pamoja na jumuiya ya MUHAS wanaungana na familia ya marehemu Emil N. Kikwilu katika kuomboleza msiba huu.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina
IMETOLEWA NA:
OFISI YA HABARI NA MAWASILIANO YA UMMA - MUHAS
29/08/2018


Hivyo makala MUHAS YATANGAZA KIFO CHA MAREHEMU PROFESA EMIL N. KIKWILU

yaani makala yote MUHAS YATANGAZA KIFO CHA MAREHEMU PROFESA EMIL N. KIKWILU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MUHAS YATANGAZA KIFO CHA MAREHEMU PROFESA EMIL N. KIKWILU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/muhas-yatangaza-kifo-cha-marehemu.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MUHAS YATANGAZA KIFO CHA MAREHEMU PROFESA EMIL N. KIKWILU"

Post a Comment