title : MHASIBU CHUO CHA USTAWI WA JAMII AHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA MITANO
kiungo : MHASIBU CHUO CHA USTAWI WA JAMII AHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA MITANO
MHASIBU CHUO CHA USTAWI WA JAMII AHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA MITANO

Aliyekuwa mhasibu wa Chuo cha ustawi wa Jamii, Gryson Mnyawami, amehukumiwa kwenda jela miaka mitano baada ya kupatikana na hata wizi wa zaidi ya sh. Milioni 9 akiwa mtumishi
Hukumu hiyo, imesomwa leo Agosti 15,2018 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Hakimu Mkazi Mkuu Janeth Mtega,
Akisoma hukumu hiyo, hakimu Mtega amesema upande wa mashtaka kupitia mashahidi wake watano wameweza kuthibitisha pasipo kuacha shaka kuwa mtuhumiwa ametenda kosa la wizi.Hata hivyo, kabla ya kusomwa kwa hukumu hiyo, Hakimu Mtega alitaka mwendesha mashtaka kusema kumbukumbu kama mshtakiwa anamakosa mengine au La
Mwendesha Mashtaka, wakili wa Serikali Janeth Magoha ameieleza mahakama kuwa, hakuna kumbukumbu za makosa kwa mshtakiwa, hili ni kosa lake la kwanza.Mheshimiwa Hakimu, sina kumbukumbu za zamani za mshtakiwa, ila naomba mahakama kutoa adhabu kali kwa kuwa kitendo cha wizi alichofanya mshtakiwa haswa akiwa kama mtumishi wa umma ni kibaya, kinaitia hasara kubwa Serikali
Wakili Janet ameongeza, suala la wizi katika Chuo cha ustawi limekuwa likitokea mara kwa mara Kitendo cha yeye kudhulumu wanafunzi siyo haki kwani ile ni hela ya walipa kodi, adhabu kali itakuwa fundisho kwake na kwa wengine wenye tabia kama hiyo
Katika utetezi wake, mshtakiwa Mnyawami, ameiomba mahakama hiyo kumpunguzia adhabu, alikubali kulipa fedha hizo taratibu lakini taasisi ndiyo ilimkatalia,Ameongeza kuwa Dada yake ni mgonjwa na mama yake ni mjane na wote wanamtegemea yeye.
Awali ilidaiwa, May 31, 2014 katika Chuo cha ustawi wa jamii kilichopo Kijitonyama wilayani Kinondoni mtuhumiwa akiwa ameajiriwa kama mhasibu wa Chuo hicho aliiba sh, 9,714,000 Mali ya muajiriwa wake ambayo ameipata kutokana na nafasi yake kazini hapo,
Hivyo makala MHASIBU CHUO CHA USTAWI WA JAMII AHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA MITANO
yaani makala yote MHASIBU CHUO CHA USTAWI WA JAMII AHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA MITANO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MHASIBU CHUO CHA USTAWI WA JAMII AHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA MITANO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/mhasibu-chuo-cha-ustawi-wa-jamii.html
0 Response to "MHASIBU CHUO CHA USTAWI WA JAMII AHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA MITANO"
Post a Comment