title : MHANDISI MTIGUMWE APONGEZA SPIDI YA UJENZI WA MAGHALA NA VIHENGE VYA KISASA
kiungo : MHANDISI MTIGUMWE APONGEZA SPIDI YA UJENZI WA MAGHALA NA VIHENGE VYA KISASA
MHANDISI MTIGUMWE APONGEZA SPIDI YA UJENZI WA MAGHALA NA VIHENGE VYA KISASA
Na Mathias Canal, WK-Ruvuma
Katibu Mkuu Wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe ameupongeza uongozi Wa Wakala Wa Taifa Wa hifadhi ya Chakula (NFRA) kwa kasi ya utekelezaji Wa ujenzi wa mradi wa maghala na Vihenge vya kisasa.
Mhandisi Mtigumwe ametoa pongezi hizo mara baada ya kutembelea na kukagua ujenzi ujenzi wa mradi huo leo Tarehe 4 Agosti 2018 katika kanda ya wakala Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma ambapo alitaja maeneo yatakayojengwa mradi huo kuwa ni pamoja na Wilaya ya Dodoma Mkoani Dodoma, Mpanda (Katavi), Songea (Ruvuma), Makambako (Njombe), Mbozi (Songwe), Sumbawanga (Rukwa), Shinyanga Mjini (Shinyanga), na Babati (Manyara).
Mradi huo ni matokeo ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Poland kusaini mkataba wa mkopo wa masharti nafuu Septemba 2015 wa Dola milioni 55 sawa na sh. bilioni 124, kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo, ambao utaongeza uwezo wa hifadhi ya chakula
Alisema wizara ya kilimo imeingia katika ujenzi huo wa maghala na vihenge vya kisasa ambao utaongeza uwezo wa kuhifadhi mahindi kutoka Tani 251,000 za sasa hadi Tani 700,000 ifikapo mwaka 2025.
Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli inahitaji watumishi wachapa kazi na kwamba wananchi na jamii kwa ujumla wake inategemea hifadhi ya chakula kilichohifadhiwa na NFRA pindi inapotokea kadhia ya ukosefu au upungufu wa chakula.
Katibu Mkuu Wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akikagua hali ya uhifadhi wa mahindi na kubaini akiba ya chakula mara baada ya kutembelea Wakala Wa Taifa wa hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Songea leo Tarehe 4 Agosti 2018.
Katibu Mkuu Wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akijadili jambo na Mratibu wa mradi wa ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa Mhandisi Imani Nzobonaliba baada ya kutembelea Wakala Wa Taifa wa hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Songea leo Tarehe 4 Agosti 2018.
Katibu Mkuu Wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akijadili jambo wakati alipotembelea na kukagua ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa katika ofisi ya Wakala Wa Taifa wa hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Songea leo Tarehe 4 Agosti 2018.
Hivyo makala MHANDISI MTIGUMWE APONGEZA SPIDI YA UJENZI WA MAGHALA NA VIHENGE VYA KISASA
yaani makala yote MHANDISI MTIGUMWE APONGEZA SPIDI YA UJENZI WA MAGHALA NA VIHENGE VYA KISASA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MHANDISI MTIGUMWE APONGEZA SPIDI YA UJENZI WA MAGHALA NA VIHENGE VYA KISASA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/mhandisi-mtigumwe-apongeza-spidi-ya.html
0 Response to "MHANDISI MTIGUMWE APONGEZA SPIDI YA UJENZI WA MAGHALA NA VIHENGE VYA KISASA"
Post a Comment