MCHENGA BBALL STARS WANYAKUA TENA UBINGWA WA SPRITE BBALL KINGS 2018

MCHENGA BBALL STARS WANYAKUA TENA UBINGWA WA SPRITE BBALL KINGS 2018 - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MCHENGA BBALL STARS WANYAKUA TENA UBINGWA WA SPRITE BBALL KINGS 2018, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MCHENGA BBALL STARS WANYAKUA TENA UBINGWA WA SPRITE BBALL KINGS 2018
kiungo : MCHENGA BBALL STARS WANYAKUA TENA UBINGWA WA SPRITE BBALL KINGS 2018

soma pia


MCHENGA BBALL STARS WANYAKUA TENA UBINGWA WA SPRITE BBALL KINGS 2018



Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Mchenga Bball Stars imefanikiwa kutetea ubingwa wake wa Sprite Bball Kings kwa mara ya pili mfululizo baada ya kufanikiwa kuwafunga wapinzani wake Flying Dribbllers kwa pointi 87 dhidi ya 76 kwenye mchezo wa game 3 ya 'best of five' za fainali uliochezwa mwishoni mwa wiki kwenye uwanja wa ndani wa taifa.

Mechi hiyo iliyoanza kwa kasi kwa pande zote, Mchenga alifanikiwa kushinda katika quarter zote nne na kuzidi kuonesha ubabe kwa timu zingine kwenye michuano ya Sprite BBall Kings.

Mchenga wamefanikiwa kuchukua ubingwa huo kwa kushinda game zote tatu mfululizo yaani (Swipe) kati ya tano za fainali hivyo kuwanyima furaha wapinzani wao Flying Dribbllers kwa mara ya pili mfululizo baada ya kuwafunga kwa aina hii hii kwenye nusu fainali ya michuano hiyo mwaka 2017.

Katika game 1 Mchenga walishinda kwa pointi 103 dhidi ya 73 za Flying Dribblers, kabla ya kushinda kwa pointi 85 kwa 65 kwenye game 2 na leo kumalizia kazi kwa ushindi wa pointi 87 kwa 76.Katika ushindi huo wa Mchenga Bball Stars mchezaji Baraka Sadick amekuwa na msaada mkubwa hali ambayo imepelekea kuibuka kama 'Most Valuable Player' wa mashindano kwa mwaka 2018.

Baraka amefunga pointi 239 katika michezo 8 aliyocheza. Katika michezo hiyo amekuwa na wastani wa kufunga pointi 30 katika kila mchezo. Katika mchezo wa leo Baraka amefunga pointi 33 kati ya 87 za timu yake.ainali hiyo ya aina yake iliweza kushuhudiwa na Rais wa Shirikisho la Kikapu (TBF) Phares Magesa akiwa na viongozi wengine na kujionea michuano hiyo ilivyokuwa na ushawishi mkubwa kwa vijana wa kitanzania.

Timu zote zimekabidhiwa zawadi zao na Rais wa TBF Phares Magesa akiwa sambamba na Katibu Mkuu wa TBF Mike Mwita ambazo ni shilingi milioni 3 kwa mshindi wa pili Flying Dribbllers, milioni mbili na tuzo kwa 'MVP' ambaye ni Baraka Sadick na milioni 10 kwa mabingwa ambao ni Mchenga Bball Stars. Sprite Bball Kings inaandaliwa na East Afarica Television chini ya udhamini wa kinywaji baridi cha Sprite.

Michuano hiyo ilianza rasmi mwaka 2017 kukiwa na timu 54 na Mchenga Bball Stars kufanikiwa kuchukua ubingwa huo kwa mara ya kwanza , msimu wa pili ulioanza mwezi June uliweza kuzikutanisha timu 51 zilizoanzia hatua ya mtoano na fainali kufanikiwa kuingia kwa timu mbili na Mchenga kutetea ubingwa wake tena.


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu (TBF) Phares Magesa akimkabiidhi kombe Nahodha wa timu ya Mchenga BBall Stars Mohamed Yusuph sambamba na hundi ya Milioni 10 baada ya kunyakua ubingwa wa pili mfululizo wa Michuano ya Sprite BBall Kings 2018 yaliyofanyika katika Uwanja wa Ndani wa Taifa Jijini Dar es Salaam
Mchezaji Baraka Sadick (aliyebebwa) akishangilia pamoja na wenzake baada ya kutangazwa kuwa mchezaji bora wa michuano hiyo ya Sprite BBall Kings 2018 (MVP) na kujinyakulia kikombe pamoja na hundi ya Milioni 2.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Nchini (TBF) Phares Magesa akimkabidhi Kikombe na hundi ya milioni 2 mchezaji bora wa mashindano ya Sprite BBall Kings 2018 (MVP) Baraka Sadick kutokea Mchenga BBall Stars katika fainali iliyofanyika Uwanja wa Ndani wa Taifa


Hivyo makala MCHENGA BBALL STARS WANYAKUA TENA UBINGWA WA SPRITE BBALL KINGS 2018

yaani makala yote MCHENGA BBALL STARS WANYAKUA TENA UBINGWA WA SPRITE BBALL KINGS 2018 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MCHENGA BBALL STARS WANYAKUA TENA UBINGWA WA SPRITE BBALL KINGS 2018 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/mchenga-bball-stars-wanyakua-tena.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MCHENGA BBALL STARS WANYAKUA TENA UBINGWA WA SPRITE BBALL KINGS 2018"

Post a Comment