title : KESI INAYOMKABILI ALIYEKUWA MHASIBU WA TAKUKURU KUSIKILIZWA AGOSTI 13, 2018
kiungo : KESI INAYOMKABILI ALIYEKUWA MHASIBU WA TAKUKURU KUSIKILIZWA AGOSTI 13, 2018
KESI INAYOMKABILI ALIYEKUWA MHASIBU WA TAKUKURU KUSIKILIZWA AGOSTI 13, 2018
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imepanga Agosti 13, 2018 kuendelea kusikiliza kesi inayomkabili aliyekuwa mhasibu wa Takukuru, Godfrey Gugai anayekabiliwa na tuhuma ya utakatishaji na kumiliki mali isiyolingana na kipato chake inayomka bili yeye na wenzake watatu.
Kesi hiyo leo Agosti 6, 2018 ilikuja kwa ajili ya shahidi Ayoub Akida wa upande wa mashtaka kuendelea kutoa ushahidi wake ambao alisimama kuutoa kutokana na kubishania kielelezo cha barua ya kufutwa kazini kwa Gugai.
Hata hivyo, wakili wa serikali kutoka Takukuru, Vitalis Peter ameeleza mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa shahidi huyo amepata udhuru.
Aidha imedaiwa wakili wa utetezi Alex Mgongolwa amefiwa na mdogo wake, Na hivyo mahakama kulazimika kuiahirisha kesi hiyo hadi Agosti 13.
Mbali na Gugai, washtakiwa wengine, ni George Makaranga, Leonard Aloys na Yasin Katera.
Washtakiwa hao wanakabiliwa na makosa 43, kati ya hayo 19 ni ya kughushi, 23 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki mali zilizozidi kipato halali.
Gugai anakabiliwa na kosa la kumiliki mali kinyume na kipato chake, ambapo alitenda kosa hilo kati ya January 2005 na Decemba 2015.
Inadaiwa akiwa jijini Dar es Salaam kama mwajiriwa wa TAKUKURU alikuwa akimiliki mali za zaidi ya Sh 3.6 bilioni ambazo hazilingani na kipato chake cha awali na cha sasa cha zaidi ya Tsh.milioni 800,huku akishindwa kuzitolea maelezo.
Hivyo makala KESI INAYOMKABILI ALIYEKUWA MHASIBU WA TAKUKURU KUSIKILIZWA AGOSTI 13, 2018
yaani makala yote KESI INAYOMKABILI ALIYEKUWA MHASIBU WA TAKUKURU KUSIKILIZWA AGOSTI 13, 2018 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KESI INAYOMKABILI ALIYEKUWA MHASIBU WA TAKUKURU KUSIKILIZWA AGOSTI 13, 2018 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/kesi-inayomkabili-aliyekuwa-mhasibu-wa.html
0 Response to "KESI INAYOMKABILI ALIYEKUWA MHASIBU WA TAKUKURU KUSIKILIZWA AGOSTI 13, 2018"
Post a Comment