WAAJIRI KUCHANGIA MFUKO KWA WAKATI

WAAJIRI KUCHANGIA MFUKO KWA WAKATI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAAJIRI KUCHANGIA MFUKO KWA WAKATI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAAJIRI KUCHANGIA MFUKO KWA WAKATI
kiungo : WAAJIRI KUCHANGIA MFUKO KWA WAKATI

soma pia


WAAJIRI KUCHANGIA MFUKO KWA WAKATI

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF) Masha Mshomba amewasisitiza waajiri wote nchini kulipa michango yao katika mfuko huo kwa wakati.

Pia ameelezea namna ambavyo mfuko huo ufurahishwa na hatua ambazo zinachukuliwa na viongozi wa ngazi za juu katika Serikali ya Awamu ya Tano ya kuhimiza wajajiri kuchangia.

Akizungumza leo katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam Mshomba amesema kuwa hamasa ambayo viongozi wa Serikali wanayo katika kuhimiza waajiri kuchangia mfuko huo imefanya waajiri wengi kuchangia kwa wakati.

“Ukweli tunapata ushirikiano mkubwa kutoka kwa viongozi wa Serikali kwa ngazi mbalimbali.Hivyo imekuwa rahisi kwa waajiri kuelewa na kutoa kuchangia mfuko.“Waajiri ambao hawachangii mfuko ni wachache na sheria inaturuhusu kuwachukulia hatua lakini tunachofanya ni kuendelea kuwahimiza na kuwalimisha na wale ambao tutaona hawataki kulipa basi tutachukua sheria,”amesema Mshomba.

Kuhusu Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi amesema ni taasisi ya hifadhi ya jamii iliyoundwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 Sheria ya fidia kwa wafanyakazi.Amesema lengo la kuanzishwa kwa mfuko huo ni kushughulikia masuala ya fidia kwa wafanyakazi waliopo katika sekta ya umma na binafsi Tanzania Bara ambao wataumia , kuugua ama kufariki kutokana na kazi wanazozifanya kwa mujibu wa mikataba ya ajira zao.

Akitaja mafao ya mfuko huo amesema kuna mafao ya Huduma ya matibabu, malipo ya ulemavu wa muda, malipo ya ulemavu wa kudumu, malipo kwa anayemhudumia mgonjwa, huduma za ukarabati na ushauri nasaha , msaada wa mazishi na malipo kwa wategemezi.

Kuhusu walengwa wa mafao Mshomba amesema walengwa ni wafanyakazi ambao wataumia au kuugua kutokana na kazi walizoajiriwa nazo.Pia wategemezi wa mfanyakazi atakayefariki kutokana na ajali au ugonjwa uliotokana na kazi.

Pamoja na hayo amesema mfuko huo umekuwa msaada mkubwa katika kuwahudumia wafanyakazi na kwamba kwa upande wao wanatumia siku 30 tu katika kulipa mafao na kubwa zaidi ambacho wanajivunia ni namna ambavyo wanatumia mtandao katika kutekeleza majukumu yao.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bw.Masha Mshomba akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Tathmini na Tiba Dk. Abdulssalaam Omary wakati alipotembelea katika banda la taasisi hiyo lililopo kwenye viwanja vya maonesho vya Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam leo, Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha, Mipango na Uwekezaji Bw. Bezil Ewala na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Bi. Laura George .
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bw.Masha Mshomba akizungumza na waandishi wa habari wa kituo cha luninga cha Chanel Ten wakati alipokuwa akieleza mikakati mbalimbali ya shirika hilo kwa ajili ya wastaafu.
Baadhi ya wafanyakazi mbalimbali wakiwa katika banda la shirika hilo tayari kwa kuhudumia wateja mbalimbali wanaotembelea katika maonesho ya Sabasaba.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bw.Masha Mshomba katikati Mkurugenzi wa Tathmini na Tiba Dk. Abdulssalaam Omary kushoto na Mkurugenzi wa Fedha, Mipango na Uwekezaji Bw. Bezil Ewala wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi walioko katika banda hilo ili kuwahudumia wananchi wanaotembelea banda hilo.
Baadhi ya wafanyakazi wakiwa katika picha ya pamoja nje ya banda hilo.



Hivyo makala WAAJIRI KUCHANGIA MFUKO KWA WAKATI

yaani makala yote WAAJIRI KUCHANGIA MFUKO KWA WAKATI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAAJIRI KUCHANGIA MFUKO KWA WAKATI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/waajiri-kuchangia-mfuko-kwa-wakati.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WAAJIRI KUCHANGIA MFUKO KWA WAKATI"

Post a Comment