title : KAMPUNI YA BRANCH YATENGA BILIONI 570 KUWASAIDIA WATANZANIA KUPITIA MIKOPO NAFUU
kiungo : KAMPUNI YA BRANCH YATENGA BILIONI 570 KUWASAIDIA WATANZANIA KUPITIA MIKOPO NAFUU
KAMPUNI YA BRANCH YATENGA BILIONI 570 KUWASAIDIA WATANZANIA KUPITIA MIKOPO NAFUU
Afisa Mtendaji Mkuu Kampuni ya Branch Matthew Plannery Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaaam.Mkurugenzi wa Kampuni ya Nefrid Afrika Charles Matondane akifafanua jambo leo jijini Dar es Salaam wakati akieleze ubora wa huduma inayotolewa na Kampuni ya Branch.
Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Kampuni ya Branch inatarajia kutoa mikopo yenye thamani ya bilioni 570 kwa njia ya huduma za kifedha kwa viwango vya juu kupitia mitandao ya simu za mkononi bila ya masharti magumu.
Kiasi hicho cha fedha kinatarajiwa kutolewa kwa watanzania kwa kipindi cha mwaka huu ambao wataomba mkopo kwa njia ya mtandao baada ya kuwa na Appy ya branch.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Afisa Mtendaji Mkuu Kampuni ya branch Matthew Plannery, amesema kuwa branch imekuwa ikitoa mikopo ya fedha kupitia simu (Smart Phone za Android) ndani ya muda mfupi.
Amesema kuwa mkopaji anaweza kukopa kuanzia shillingi 5,000 hadi I,000,000 ndani ya dakika tatu baada kutuma maombi na kukubaliwa.
"Kampuni ya branch inatoa fursa ya kupata mkopo chap-chap kupitia simu, haihitaji kuonana ana kwa ana na mtoa huduma au kuwa na dhama, kujaza fomu za karatasi" amesema Plannery.
Plannery ameeleza kuwa kadri ambavyo mteja kampuni ya branch anavyofanya marejesho ya mkopo wake ndivyo anavyozidi kujifungulia fursa ya kupata mkopo mkubwa zaidi na masharti rahisi.
Meneja Mkuu Kampuni ya Branch, Afrika Mashariki Dan Karuga, amesema kuwa mikopo yao inatolewa na kulipwa kupitia huduma za fedha kupitia mitandao ya simu kama TigoPesa, M-PESA pamoja na Aitel.
Karuga amefafanua kuwa hakuna masharti magumu wakati unataka kuomba mkopo ila mkopaji anapaswa kuwa na Appy ya Branch ambayo inapatika pray store.
Amesema kuwa zaidi asilimia 75 ya wateja wanatumia mikopo ya branch kuwasaidia kuanzisha au kukuza biashara kupitia branch.
"Branch haina vikwazo juu ya matumizi ya mkopo wako, wateja wanaouhuru wa kufanya maamuzi yao ya kifedha" amesema Karuga.
Kampuni ya branch utoa mikopo kwa wateja wake bila kujali historia yao ya huduma za kibenki kwa kufanyia uchambuzi na sifa zao za kupata mkopo.
Karuga amesema kutokana na ruhusa ya mteja, mfumo wa kimahesabu wa branch unaweza kuchambua maelfu ya taarifa na kutengeneza makadilio ambayo mteja anafaa kupokea.
"Taarifa binafsi za wateja wetu hulindwa kwa kutumia mifumo ya hali ya juu ya kusalama kimtandaoni na usimbaji-fiche ili kuhakikisha usalama" amesema Karuga.
Kampuni ya branch mpaka sasa hapa nchini imekwishatoa mikopo ya zaidi ya bilioni I2, lakini bado inaendelea kukua kwa kasi kwa kubuni na kuingiza bidhaa pamoja na huduma mpya ili kuongeza ubora wa huduma zao.
Mwaka huu kampuni ya Branch inatarajia kukopesha wateja wake bilioni 570 ikiwa na mipango kuwasaidia watanzania kifedha kupitia huduma ya kimtandao ambao inayoongoza barani Afrika.
Kampuni ya Branch imelenga kuisaidia jamii kiuchumi kupitia mikopo kwa njia ya mitandao ya simu za mkononi, ofisi zake kampuni hiyo zipo Marekani, Kenya, Nigeria pamoja na Mexico.
Hivyo makala KAMPUNI YA BRANCH YATENGA BILIONI 570 KUWASAIDIA WATANZANIA KUPITIA MIKOPO NAFUU
yaani makala yote KAMPUNI YA BRANCH YATENGA BILIONI 570 KUWASAIDIA WATANZANIA KUPITIA MIKOPO NAFUU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KAMPUNI YA BRANCH YATENGA BILIONI 570 KUWASAIDIA WATANZANIA KUPITIA MIKOPO NAFUU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/kampuni-ya-branch-yatenga-bilioni-570.html
0 Response to "KAMPUNI YA BRANCH YATENGA BILIONI 570 KUWASAIDIA WATANZANIA KUPITIA MIKOPO NAFUU"
Post a Comment