title : DKT TIZEBA AAGIZA WAKAGUZI WA VIUATILIFU KULINDA MASLAHI YA TAIFA
kiungo : DKT TIZEBA AAGIZA WAKAGUZI WA VIUATILIFU KULINDA MASLAHI YA TAIFA
DKT TIZEBA AAGIZA WAKAGUZI WA VIUATILIFU KULINDA MASLAHI YA TAIFA
Na Mathias Canal, WK-Morogoro
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba leo tarehe 5 Agosti 2018 amefungua rasmi mafunzo ya wakaguzi wa viuatilifu yaani mimea na mazao katika hafla iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha kilimo (SUA) Mkoani Morogoro ambapo asilimia 99 ya washiriki wanatoka katika vituo vya ukaguzi wa mazao mipakani vikiwemo vya nchi kavu, bandarini na viwanja vya ndege.
Katika mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu katika Ukanda wa Kitropiki (Tropical Pesticide Research Institute - TPRI), Waziri Dkt Tizeba ameagiza washiriki hao Kulinda maslahi ya wakulima, walaji na Taifa kwa ujumla dhidi ya wafanyabiashara wachache wa viuatilifu wanaotaka kutajirika kwa kutuletea viuatilifu vilivyo chini ya kiwango.
Waziri huyo anayeshughulikia sekta ya kilimo nchini ameyasema hayo kwa msisitizo mkubwa huku akiwataka kutekeleza wajibu wao wa ukaguzi wa viatilifu kwa umakini, uaminifu na uadilifu mkubwa kwa kutumia Sheria na Kanuni zilizopo. Amesisitiza kuwa wataalamu hao wanapaswa kuitetea maslahi ya nchi pale inapohitajika kwa kutumia kwa umakini mkubwa kwa utashi wa Sheria na Kanuni zinazotakiwa ikiwa ni pamoja na taratibu nyingine za kisheria katika kuhusisha watumishi wengine wa Serikali kama waendesha mashtaka wa Serikali na askari.
Pia, aliwataka Wakaguzi kutoka Makao Makuu ya Wizara na Taasisi ya TPRI kuangalia namna ya kuunganisha shughuli zinazofanywa kati ya Kitengo cha afya ya mimea (PHS) na TPRI katika kuwasimamia na kuwaongoza wakaguzi kutoka katika vituo vyetu vya mipakani ili watekeleze majukumu yao kwa ufanisi na uadilifu kwa kuwapatia vitendea kazi pale fursa zinapopatikana kwa kuzingatia mahitaji.
Mgeni rasmi-Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akizungumza wakati wa mkutano wa ufunguzi wa mafunzo ya wakaguzi wa viuatilifu kwenye hafla iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha kilimo (SUA) Mkoani Morogoro leo Tarehe 5 Agosti 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akisisitiza ufanisi kazini wakati akizungumza kwenye mkutano wa ufunguzi wa mafunzo ya wakaguzi wa viuatilifu kwenye hafla iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha kilimo (SUA) Mkoani Morogoro leo Tarehe 5 Agosti 2018.
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu katika Ukanda wa Kitropiki (Tropical Pesticide Research Institute - TPRI) Dkt Margaret Mollel akitoa taarifa ya mafunzo ya wakaguzi wa viuatilifu mbele ya mgeni rasmi Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba kwenye hafla iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha kilimo (SUA) Mkoani Morogoro leo Tarehe 5 Agosti 2018.
Picha ya pamoja baada ya kumalizika mkutano wa ufunguzi wa mafunzo ya wakaguzi wa viuatilifu kwenye hafla iliyofanyika Chuo Kikuu cha kilimo (SUA) Mkoani Morogoro leo Tarehe 5 Agosti 2018.

Hivyo makala DKT TIZEBA AAGIZA WAKAGUZI WA VIUATILIFU KULINDA MASLAHI YA TAIFA
yaani makala yote DKT TIZEBA AAGIZA WAKAGUZI WA VIUATILIFU KULINDA MASLAHI YA TAIFA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DKT TIZEBA AAGIZA WAKAGUZI WA VIUATILIFU KULINDA MASLAHI YA TAIFA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/dkt-tizeba-aagiza-wakaguzi-wa.html
0 Response to "DKT TIZEBA AAGIZA WAKAGUZI WA VIUATILIFU KULINDA MASLAHI YA TAIFA"
Post a Comment