title : TUKIO LA KUHAMIA KWA MAKUNDI YA NYUMBA MBUGA YA SERENGETI, NIHALISI WATALII WAONGEZA MUDA KUSHUHUDIA.
kiungo : TUKIO LA KUHAMIA KWA MAKUNDI YA NYUMBA MBUGA YA SERENGETI, NIHALISI WATALII WAONGEZA MUDA KUSHUHUDIA.
TUKIO LA KUHAMIA KWA MAKUNDI YA NYUMBA MBUGA YA SERENGETI, NIHALISI WATALII WAONGEZA MUDA KUSHUHUDIA.
Watalii wakiwa kando ya Mto Mara katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ,eneo la Kogatende wakishuhudia tukio kubwa la kuhama kwa Makundi Makubwa ya Nyumbu wakivuka mto kutoka Hifadhi ya Masai Mara nchini Kenya kuingia Hifadhi ya Taifa ya
Serengeti
Baadhi ya Watalii wamelazimika kuongeza siku za kukaa katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa ajili ya kushuhudia tukio hilo la aina yake ambalo hutokea kila mwaka .
Kundi kubwa la Nyumbu likiwa katika maandalizi ya kuvuka Mto Mara kuingia Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Magari yaliyobeba Watalii yakiwa yameegeshwa kando ya Mto Mara kusubiri tukio la kuvuka kwa Makundi ya Nyumbu katika Mto Mara kuingia Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Mamba wakiwa Mto Mara katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakiwa katika mawindo ya Mnyama Nyumbu wakati akivuka.
Mnyama Pundamlia wakiwa upande wa pili mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ,tunaweza sema ni kama wako hapo kwa ajili ya mapokezi ya Nyumbu wanarudi kutoka katika Hifadhi ya Masai Mara nchini Kenya.
Eneo la Mto Mara ambapo Watalii wakingojea tukio la kuvuka kwa Makundi ya Nyumbu.
Na Dixon Busagaga.
Hifadhi ya Taifa ya Serengeti iliyopo Mkoani Mara,imeendelea kuwa maarufu Duniani na kuvutia watalii wengi zaidi kutoka maeneo mbalimbali ya Dunia kwa ajili ya kujionea tukio la kila mwaka la kuhama kwa Makundi makubwa ya Nyumbu kutoka Hifadhi ya Masai Mara nchini Kenya na kuingia Serengeti.
Tukio hili ambalo hutokea kuanzia mwezi Julai na wageni kulipa jina la “Great Wildebeest Migration” mwaka huu linatajwa kuvutia watalii wengi zaidi huku wengine wakilazimika kuongeza siku za kukaa katika Hifadhi ya Serengeti wakingojea kushuhudia tukio hilo.
Mwandishi ameshuhudia Msururu wa Magari ya kubeba watalii yakiwa na wageni kando ya Mto Mara kusubiri kujionea hali inavyokuwa wakati wanyama hao wakivuka kwa makundi kutoka upande mmoja wao kuingia Hifadhi ya Serengeti.
Eneo la Mto Mara ambapo Wanyama hawa wamekuwa wakivuka linatajwa kuwa na Vivuko 10 hali inayochangia waongoza watalii kufuata mwenendo wa Nyumbu kwa sababu si rahisi kufahamu wapi wataelekea kuvuka jambo ambalo hutumia zaidi ya saa 5 hadi 7 kungojea tukio hilo.
Tukio la misafara ya makundi ya wanyama hao kuhama na kurudi hubadilika kila mwaka kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na kiwango cha maji katika mto mara hata hivyo limeendelea kuwa kivutio kikubwa kwa wageni.
Kivutio kikubwa katika misafara ya wanyama hao ambao wamekuwa wakiondoka nchini kila mwaka kuanzia mwezi mey na kurudi kuanzia mwezi julay ni namna wanavyovuka mto mara na jinsi wanavyokabiliana na wanyama wengine ndani ya mto huo wakiwemo Mamba
Hivyo makala TUKIO LA KUHAMIA KWA MAKUNDI YA NYUMBA MBUGA YA SERENGETI, NIHALISI WATALII WAONGEZA MUDA KUSHUHUDIA.
yaani makala yote TUKIO LA KUHAMIA KWA MAKUNDI YA NYUMBA MBUGA YA SERENGETI, NIHALISI WATALII WAONGEZA MUDA KUSHUHUDIA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TUKIO LA KUHAMIA KWA MAKUNDI YA NYUMBA MBUGA YA SERENGETI, NIHALISI WATALII WAONGEZA MUDA KUSHUHUDIA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/tukio-la-kuhamia-kwa-makundi-ya-nyumba.html
0 Response to "TUKIO LA KUHAMIA KWA MAKUNDI YA NYUMBA MBUGA YA SERENGETI, NIHALISI WATALII WAONGEZA MUDA KUSHUHUDIA."
Post a Comment