DIWANI VIGWAZA AANZA ZIARA YA KUTEMBELEA MIRADI VIJIJINI

DIWANI VIGWAZA AANZA ZIARA YA KUTEMBELEA MIRADI VIJIJINI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DIWANI VIGWAZA AANZA ZIARA YA KUTEMBELEA MIRADI VIJIJINI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DIWANI VIGWAZA AANZA ZIARA YA KUTEMBELEA MIRADI VIJIJINI
kiungo : DIWANI VIGWAZA AANZA ZIARA YA KUTEMBELEA MIRADI VIJIJINI

soma pia


DIWANI VIGWAZA AANZA ZIARA YA KUTEMBELEA MIRADI VIJIJINI

NA MWAMVUA MWINYI,VIGWAZA

DIWANI wa kata ya Vigwaza ,Bagamoyo , Pwani ,Mohsin Bharwani (CCM),amechangia mabati 242, mifuko ya saruji 100 na matofali 3,000 vyenye thamani takriban sh.milioni 12 katika kijiji cha Chamakweza,Mnindi na kitongoji cha Serengeti.

Amesema ametoa vifaa hivyo vya ujenzi ,ili kutekeleza ilani ya CCM na kuunga mkono juhudi za wananchi katika miradi wanayoiibua na miradi ya serikali.Bharwani alitoa michango hiyo, katika ziara yake ya kutembelea baadhi ya miradi ya maendeleo katika vijiji vilivyopo kata ya Vigwaza ,ambapo ameanza kwenye vijiji vya Chamakweza,Mnindi na kitongoji cha Serengeti.

"Shule ya msingi Chamakweza ambayo darasa moja na ofisi havina mabati nimetoa mabati 96 yenye thamani ya sh.milioni 2.8 " #"Katika kitongoji cha Serengeti kilio cha wananchi ni kupata shule ya awali ,na tunashukuru halmashauri imeleta mshauri kutoka idara ya elimu msingi kwenye mkutano huu kwani tumepata nafasi ya kumueleza adhma yetu na kutupa maelekezo" alifafanua .

Kutokana na hilo ,Bharwani alitoa ,mifuko ya saruji 50 ,matofali 2,000 ,licha ya kuendelea kwa hatua nyingine zitakazozingatia vigezo vinavyotakiwa ili kufikia hatua ya kupata kibali cha kujenga na kuwa na shule si tu ya awali bali shule ya msingi.Akiwa kijiji cha Mnindi ambacho kinaendelea na ujenzi wa zahanati alisema ,"wakati ujenzi ulipoanza alichangia mifuko 50 na kwasasa amechangia mabati 96 yenye thamani ya milioni 2.8.

"Serikali inafanya mambo makubwa kwa utkeleza miradi mbalimbali ya reli ,barabara,umeme,afya,elimu na maji hivyo lazima viongozi wa chini tuunge mkono juhudi hizo ,na kushirikiana na rais Dk.John Magufuli kutatua kero mbalimbali kuanzia ngazi ya chini ""Rais karudisha imani kwa wananchi na wadau wanaoshiriki kusaidia masuala mbalimbali, katupa jeuri CCM kutokana na kutekeleza ahadi na ilani kwa kugusa kila eneo ili kuinua maendeleo na uchumi ." alisema Bharwani.

Bharwani aliwataka ,viongozi wa kuchaguliwa na watendaji wengine kuunganisha nguvu na ya wananchi kuisaidia serikali ya CCM ili kipiga hatua zaidi wakati nchi ikielekea kwenye uchumi wa kati .Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi wa halmashauri ,Erasto Meshack kutoka idara ya elimu msingi alisema ,kwa mujibu wa miongozo kigezo cha kwanza ili shule iitwe shule inapaswa kujengwa katika eneo lisilozidi hekari kumi . .

Alieleza ,ili shule iweze kufunguliwa isipungue majengo sita,stoo,vyoo vya walimu ,wanafunzi na nyumba za walimu.Nae ,mwenyekiti wa kijiji cha Vigwaza Ramadhani Kirumbi, alimshukuru diwani huyo kwa michango yake anayojitolea ,kwani kutoa ni moyo .Alisema endapo mradi wa ujenzi wa shule ya awali ya Sekibwa kitongoji cha Serengeti ukifanikiwa utawasaidia watoto ambao hutembea zaidi ya km.tano kufuata elimu hiyo nje ya eneo hilo .Mwenyekit wa CCM kata ya Vigwaza ,Shederi Mkole ,alimpongeza Bharwani kwa kujitoa kwake kutekeleza ilani ya CCM.
DIWANI wa kata ya Vigwaza , Mkoani Pwani ,Mohsin Bharwani (CCM),akizungumza katika kijiji cha Chamakweza wakati alipofanya ziara yake katika kijiji hicho ,kijiji cha Mnindi na kitongoji cha Serengeti.(picha na Mwamvua Mwinyi)
DIWANI wa kata ya Vigwaza , Mkoani Pwani ,Mohsin Bharwani (CCM),akizungumza wakati alipotembelea baadhi ya ujenzi  wa madarasa katika kijiji cha Chamakweza wakati alipofanya ziara yake katika kijiji hicho ,kijiji cha Mnindi na kitongoji cha Serengeti.
Mkazi wa Chamakweza ,Philemon Molel akimshukuru diwani wa kata ya Vigwaza ,Mohsin Bharwani wakati alipokwenda kutembelea miradi na kijijini hapo ,kijiji cha Mnindi na kitongoji cha Serengeti. (Picha na Mwamvua Mwinyi).


Hivyo makala DIWANI VIGWAZA AANZA ZIARA YA KUTEMBELEA MIRADI VIJIJINI

yaani makala yote DIWANI VIGWAZA AANZA ZIARA YA KUTEMBELEA MIRADI VIJIJINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DIWANI VIGWAZA AANZA ZIARA YA KUTEMBELEA MIRADI VIJIJINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/diwani-vigwaza-aanza-ziara-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "DIWANI VIGWAZA AANZA ZIARA YA KUTEMBELEA MIRADI VIJIJINI"

Post a Comment