title : DC atoa agizo kwa Wenyeviti wa Mtaa wilaya ya Ilala na Watendaji
kiungo : DC atoa agizo kwa Wenyeviti wa Mtaa wilaya ya Ilala na Watendaji
DC atoa agizo kwa Wenyeviti wa Mtaa wilaya ya Ilala na Watendaji
Mwambawahabari
Na Heri Shaban
MKUU wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema ametoa agizo kwa Wenyeviti wa Serikali ya Mtaa na Watendaji wote katika wilaya ya Ilala kuorodhesha majina ya Wageni wote wanaohamia katika mtaa kuweka daftari maalum la wageni .
Mjema alitoa agizo hilo Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa Habari, wakati wa kutoa majumuisho ya ziara yake iliyomalizika Tarafa ya Ukonga.
"Nawaagiza Wenyeviti wa Serikali ya Mtaa na maofisa Watendaji kila mtu asimamie majukumu yake ikiwemo suala la ulinzi na usalama katika mtaa muhakikishe mna orodha ya watu wote wageni ambao wanaingia kila siku katika maeneo ya mtaa wenu ili kupunguza wimbi la wahamiaji haramu"alisema Mjema
Mjema alisema Wenyeviti wote mkitumia taratibu huu ndani ya wilaya ya Ilala tutakuwa tumepunguza wimbi la wageni ambao wanapelekea kusumbua wananchi wa Wilaya hiyo kwa vitendo viovu nyakati tofauti.
Alisema kila MWENYEKITI kuweka daftari la kutambua wananchi wao Yale wanayofanya taratibu wa kuripoti kwa MWENYEKITI na kueleza shughuli zao katika mtaa iwe zoezi endelevu.
Aliagiza wananchi kutoa ushirikiano kwa wenyeviti wa Mtaa na watendaji kwa watu ambao wanapanga katika makazi yao kuwa na utamburisho maalum ili Wilaya ya Ilala iweze kuwa Salama na kutokomeza vitendo viovu.
Pia aliagiza Watendaji wa Wilaya ya Ilala kila mmoja kusimamia majukumu yake katika kufanya kazi kwa weledi na kusikiliza kero za wananchi na kuwahudumia.
Akizungumzia ziara ya Tarafa ya Ukonga alisema katika ziara hiyo alipokea maswali ya wananchi ya kero na kuyapatia majibu ya mengine ya Wizara yanamsubiri WAZIRI wa ardhi kwa ajili ya kuyatatua.
Alisema katika ziara hiyo zimeibuka kero za Afya, Ulinzi na Usalama ,Elimu na miundo mbinu ambapo aliagiza Ulinzi Shirikishi kila Kata waanzishe pia alimuagiza Mganga Mkuu wa MANISPAA hiyo kutatua kero za Sekta ya AFYA.
Alitoa rai kwa Watumishi na Watendaji wa wilaya ya Ilala katika idara zao za Serikali kuakikisha wanabuni mbinu na mikakati ya kuongeza kasi ya kutatua matatizo ya wananchi.
Pia aliwataka Watendaji wa Wilaya ya Ilala wasikae ofisini badala yake washuke kwa wananchi kushughulikia kero na matatizo yao kwa kuzingatia mizani ya uadilifu na uaminifu kama mwakilishi wa Rais wa awamu ya tano katika wilaya ya Ilala nitawachukulia hatua watendaji wazembe wasiopenda kutimiza wajibu wao.
Alisema ziara hiyo Mara baada kumalizika tarafa la Ukonga itafanyika SEGEREA na Ilala,
Hivyo makala DC atoa agizo kwa Wenyeviti wa Mtaa wilaya ya Ilala na Watendaji
yaani makala yote DC atoa agizo kwa Wenyeviti wa Mtaa wilaya ya Ilala na Watendaji Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC atoa agizo kwa Wenyeviti wa Mtaa wilaya ya Ilala na Watendaji mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/dc-atoa-agizo-kwa-wenyeviti-wa-mtaa.html
0 Response to "DC atoa agizo kwa Wenyeviti wa Mtaa wilaya ya Ilala na Watendaji"
Post a Comment