HOSPITAL YA MSOGA YAPOKEA MSAADA WA VIFAA

HOSPITAL YA MSOGA YAPOKEA MSAADA WA VIFAA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa HOSPITAL YA MSOGA YAPOKEA MSAADA WA VIFAA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : HOSPITAL YA MSOGA YAPOKEA MSAADA WA VIFAA
kiungo : HOSPITAL YA MSOGA YAPOKEA MSAADA WA VIFAA

soma pia


HOSPITAL YA MSOGA YAPOKEA MSAADA WA VIFAA

Mwakilishi kutoka Tanzania Health Promotion Support (THPS) ,Sisty Moshi akimkabidhi mbunge wa Chalinze ,Ridhiwani Kikwete msaada wa vifaa mbalimbali vilivyogharimu milioni 48.412 katika hospital ya wilaya ya Msoga.
Mganga mkuu wa halmashauri ya Chalinze ,Rahim Hangai akimkabidhi taarifa ya hospital ya wilaya ya Msoga, mwakilishi kutoka THPS, Sisty Moshi wakati wa makabidhiano ya vifaa katika hospital hiyo .

NA MWAMVUA MWINYI, CHALINZE

WADAU wa afya Tanzania Health Promotion Support (THPS) ,wametoa msaada wa vifaa mbalimbali vilivyogharimu milioni 48.412 katika hospital ya wilaya ya Msoga,Chalinze Mkoani Pwani. Kati ya vifaa vilivyotolewa ni pamoja na mabenchi za wagonjwa 30, meza za ofisi kumi ,viti vya ofisini 12 ,makabati ya kuhifadhia nyaraka matatu na stool kwa ajili ya maabara 13.#

Akikabidhi vifaa hivyo kwa mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete ,mganga mkuu wa halmashauri ya Chalinze na uongozi wa hospital hiyo, mwakilishi kutoka THPS ,Sisty Moshi alisema ,wamewezesha vifaa hivyo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika sekta hiyo. Alieleza ,kuanzia 2016/2018 wameshatoa vifaa tiba na samani zenye thamani zaidi ya milioni 761.508  mkoani Pwani, kati ya hivyo vifaa vilivyogharimu milioni 236.647.568 vilipelekwa Chalinze.

"Katika mradi huu wa kusaidia kuzuia maambukizi mapya ya VVU ,kutoa huduma,tiba na msaada wa kisaikolojia kwa ufadhili wa serikali ya Marekani , sisi tunafanya kazi katika mikoa ya Kigoma,Pwani na visiwa vya Zanzibar"

"Ufadhili huu unatokana na makubaliano kati ya serikali ya Tanzania na Marekani kufuatana na malengo ya kitaifa " alifafanua Moshi.

Awali akitoa taarifa ya hospital ya wilaya ya Msoga ,mganga mkuu wa halmashauri ya Chalinze ,Rahim Hangai ,alisema tarehe 12/10/2017 waziri wa afya ,maendeleo ya jamii ,jinsia ,wazee na watoto aliridhia na kutoa kibali cha kituo cha afya Msoga kuwa hospital ya wilaya. Alisema lakini bado inakabiliwa na ukosefu wa jengo la utawala,ukosefu wa gari kwa ajili ya shughuli za kiutawala,upungufu wa watumishi na chumba cha kuhifadhia maiti.

Changamoto nyingine ni ukosefu wa jengo la maabara ,jengo la tiba na mafunzo kwa watu wanaoishi na VVU (CTC),jengo la mionzi ,ukosefu wa mashine ya X-ray ya ziada na chumba cha daktari na wodi ya wagonjwa wa akili. Hangai, alisema vituo vya afya na hospital hiyo ,vimekuwa vikipokea majeruhi wengi wa ajali za barabarani kwa takwimu za julai 2016-juni 2017 vimepokea majeruhi 799 na wagonjwa waliokuwa na dharula 5,477 na wajawazito 4,678 .

Akikabidhiwa vifaa hivyo ,Ridhiwani aliwashukuru wadau hao na kuomba wadau wengine wasiwachoke kuendelea kuisaidia changamoto ambazo zinazoikabili hospital ya Msoga. Ridhiwani alielezea kuwa ,halmashauri ya Chalinze inapitiwa na barabara kuu tatu ikiwemo Dar-es-salaam -Chalinze-Arusha,Chalinze -Msata-Arusha na Bagamoyo-Msata-Arusha. Alibainisha, vituo vya afya vilivyopo katika halmashauri hiyo vimekuwa vikipokea majeruhi wengi wa ajali za barabarani na magonjwa mengine.


Hivyo makala HOSPITAL YA MSOGA YAPOKEA MSAADA WA VIFAA

yaani makala yote HOSPITAL YA MSOGA YAPOKEA MSAADA WA VIFAA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala HOSPITAL YA MSOGA YAPOKEA MSAADA WA VIFAA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/hospital-ya-msoga-yapokea-msaada-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "HOSPITAL YA MSOGA YAPOKEA MSAADA WA VIFAA"

Post a Comment