title : Bodi ya maji bonde la mto Pangani yajenga kituo cha polisi Sakale-Muheza
kiungo : Bodi ya maji bonde la mto Pangani yajenga kituo cha polisi Sakale-Muheza
Bodi ya maji bonde la mto Pangani yajenga kituo cha polisi Sakale-Muheza
Bodi ya maji mto pangani yajenga kituo cha polisi katika kitongoji cha Kwelusanga kijiji cha Sakale kata ya Mbomole baada ya changamoto za uchimbaji madini kukithiri katika chanzo cha maji cha mto Zigi na katika hifadhi za mazingira.
Akisoma taarifa ya Ujenzi wa kituo cha polisi Agosti 21, 2018 Bi Arafa Magidi kaimu Afisa bonde la Pangani, amesema bodi ya maji bonde la mto Pangani limejenga kituo hicho kupitia mkandarasi Kumba Quality Contractors kwa gharama ya Tsh. 76,088,000/= (Milioni sabini na sita na elfu themanini na nane tu.) ambazo ni mchango wa pamoja wa Serikali ya Tanzania na wadau wa maendeleo.
Ameongeza kuwa kituo hiki kina vyumba viwili vya mahabusu, mahabusu ya wanaume na mahabusu ya wanawake, ofisi ya polisi, maliwato mbili (vyoo), na sehemu ya kupokelea malalamiko.
Akikabidhiwa kituo hicho Mkuu wa Wilaya muheza Mhe. Mhandisi Mwanasha Tumbo amesema, Kituo hiki kitawasaidia wananchi wa Sakale kuimarisha hali ya ulinzi na usalama kwa raia na mali zao, pia kuwasogezea huduma wananchi karibu kwani kituo cha awali kipo mbali sana na kijiji chao.
Pia aliwahasa wananchi wa Sakale kuendelea kuhifadhi mazingira na vyanzo vya maji kwa kuhakikisha hakuna uchimbaji wa madini utakao endelea katika kijiji hicho. “Kila mmoja awe mlinzi wa mwenzie, tuendelee kuwaondoa watu wanaoharibu mazingira” Alisema Tumbo.
Mhe. Mwanasha Tumbo(wakatikati) akishuhudia tukio la kusaini mkataba wa makabidhiano ya kituo cha polisi kati ya Mwenyekiti wa bodi la bonde la mto Pangani Ndugu Segule Segule na Kaimu Kamanda Mkuu wa Polisi Tanga Ndugu Lissu Jingi
Picha ya pamoja.
Hivyo makala Bodi ya maji bonde la mto Pangani yajenga kituo cha polisi Sakale-Muheza
yaani makala yote Bodi ya maji bonde la mto Pangani yajenga kituo cha polisi Sakale-Muheza Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Bodi ya maji bonde la mto Pangani yajenga kituo cha polisi Sakale-Muheza mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/bodi-ya-maji-bonde-la-mto-pangani.html
0 Response to "Bodi ya maji bonde la mto Pangani yajenga kituo cha polisi Sakale-Muheza"
Post a Comment