title : Balozi wa Kuwait Aahidi Kuwasaidia Watoto Wenye Saratani Muhimbili
kiungo : Balozi wa Kuwait Aahidi Kuwasaidia Watoto Wenye Saratani Muhimbili
Balozi wa Kuwait Aahidi Kuwasaidia Watoto Wenye Saratani Muhimbili
Jasem Al - Najem akimkabidhi zawadi mmoja wa kina mama, Martha John Zakaria anayemuuguza mtoto wake katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Kushoto ni Naibu Mwenyekiti wa Red Crescent kutoka Kuwait, Anwar Alhasawi na mwakilishi wa Jumuiya ya Red Crescent, Mayouf Alenezi.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jasem Al-Najem akizungumza na wazazi wa watoto ambao wanatibiwa saratani katika hospitali hiyo. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati-Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Suleiman Saleh na Naibu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Red Crescent kutoka Kuwait, Anwar Alhasawi.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jasem Al-Najem ametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kuahidi kuwasaidia watoto wenye saratani ambao wanatibiwa katika hospitali hiyo.
Katika ziara hiyo balozi huyo alimtaka Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tumaini la Maisha (TLM) katika hospitali hiyo, Dkt. Trish Scanlan kumwandikia mahitaji ambayo watoto hao wanapaswa kupatiwa ili aweze kushiriki katika kuwapatia tiba pamoja na mambo mengine.
Balozi huyo aliongozana na Naibu Mwenyekiti wa Red Crescent kutoka Kuwait, Anwar Alhasawi, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati-Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki , Suleiman Salehe pamoja na pamoja na viongozi mbalimbali wa Lions Club ambayo imekuwa ikiwasadia watoto hao mahitaji mbalimbali.
Pia, balozi huyo alitembelea watoto wenye saratani katika jengo la watoto pamoja na kuwapatia zawaidi mbalimbali ikiwamo vifaa vya kuchezea.
Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa mwezi imekuwa ikipokea wastani wa watoto 30 hadi 40 wenye saratani ya aina mbalimbali. Wengi wa watoto wanaopokelewa wamekuwa wakisumbuliwa na saratani ya damu, jicho, figo na saratani ya matezi.
Hivyo makala Balozi wa Kuwait Aahidi Kuwasaidia Watoto Wenye Saratani Muhimbili
yaani makala yote Balozi wa Kuwait Aahidi Kuwasaidia Watoto Wenye Saratani Muhimbili Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Balozi wa Kuwait Aahidi Kuwasaidia Watoto Wenye Saratani Muhimbili mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/balozi-wa-kuwait-aahidi-kuwasaidia_1.html
0 Response to "Balozi wa Kuwait Aahidi Kuwasaidia Watoto Wenye Saratani Muhimbili"
Post a Comment