title : RAIS MAFUGULI: MAENDELEO HAYANA CHAMA WALA KABILA
kiungo : RAIS MAFUGULI: MAENDELEO HAYANA CHAMA WALA KABILA
RAIS MAFUGULI: MAENDELEO HAYANA CHAMA WALA KABILA
Mwambawahabari
Na Immaculate Makilika-MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli alisema kuwa maendeleo hayana chama wala kabila na hivyo viongozi huteuliwa kushika nafasi mbalimbali kutokana na uwezo wao wa utendaji kazi pamoja na uadilifu wao.
Rais Magufuli aliyasema hayo leo wakati wa hafla ya uapisho wa Wakuu wa mikoa 4, Makatibu Wakuu 2, Manaibu Katibu Wakuu 2 na Makatibu Tawala wa Mikoa 13 Ikulu jijini Dar es salaam, ambapo aliwataka viongozi hao kutekeleza vyema wajibu wao katika kuwaletea maendeleo wananchi
“Nambiwa kuwa nimechagua wapinzani, kwa Tanzania tunayoijenga ya umoja tukianza kwenda kwa vyama na makabila hatutafika, tuchague viongozi kwa utendaji wao wa kazi”Alisema Rais Magufuli.
Aliongeza kuwa “Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kasilikizeni wananchi na mkashughulikie kutatua matatizo ya wananchi katika maeneo yenu”
Aidha, Rais Magufuli alionesha kutofurahishwa na hali ya migogoro inayotokea katika maeneo mbalimbali nchini , ambayo inaweza kutatuliwa na viongozi wa maeneo hayo, ambapo amewataka viongozi hao kuwa chachu ya kutatua kero za wananchi.
Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan aliwataka viongozi hao kufanya kazi kwa bidii na kusimamia kikamilifu ukusanyaji wa mapato na matumizi katika halmashauri zao.
“ Kasimamieni kiapo hiki mlichoapa, mkawe na uhusiano mzuri na mtakao wakuta kule lakini pia nawataka mkafanye kazi sambamba na kutekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi” alisema Makamu wa Rais Samia
Naye, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliwapongeza viongozi hao walioapishwa na kusema kuwa Rais amewaamini na ni dalili watafanyakazi katika kutumikia taifa kwa uadilifu.
“ Anzeni kujifunza, mtakayoyakuta ofisini, jukumu lenu wote ni kusimamia kikamilifu shughuli za mbalimbali za serikali zitakazo chochea maendeleo ya wananchi kwa ngazi zote” amesema Waziri Mkuu.
Hafla hiyo ya uapisho kwa viongozi hao wa umma, ilihudhuriwa na viongozi mbali wakiwemo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jaffo, Jaji Kiongozi Dkt. Elieza Felshi , Wakuu wa Mikoa, viongozi wa dini pamoja na viongozi wa vyama vya siasa.
Hivyo makala RAIS MAFUGULI: MAENDELEO HAYANA CHAMA WALA KABILA
yaani makala yote RAIS MAFUGULI: MAENDELEO HAYANA CHAMA WALA KABILA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RAIS MAFUGULI: MAENDELEO HAYANA CHAMA WALA KABILA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/rais-mafuguli-maendeleo-hayana-chama.html
0 Response to "RAIS MAFUGULI: MAENDELEO HAYANA CHAMA WALA KABILA"
Post a Comment