BAKWATA yawataka Wanaomiliki Mali za Waislam kwa njia isiyo ya halali kuzirudisha

BAKWATA yawataka Wanaomiliki Mali za Waislam kwa njia isiyo ya halali kuzirudisha - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa BAKWATA yawataka Wanaomiliki Mali za Waislam kwa njia isiyo ya halali kuzirudisha, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : BAKWATA yawataka Wanaomiliki Mali za Waislam kwa njia isiyo ya halali kuzirudisha
kiungo : BAKWATA yawataka Wanaomiliki Mali za Waislam kwa njia isiyo ya halali kuzirudisha

soma pia


BAKWATA yawataka Wanaomiliki Mali za Waislam kwa njia isiyo ya halali kuzirudisha



Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Kiislamu Tanzania (BAKWATA) SHEKHE Nuhu Jabir akitoa taarifa katika baraza la Idd El haji lililofanyika Kitaifa VINGUNGUTI Wilaya ya Ilala (Picha na Heri Shaban)

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga TAIFA (JKT) Husein Mwinyi akisalimiana na Mashekhe mbalimbali Dar es salaam Jana katika Baraza la sikukuu ya Idd El Haj lililoandaliwa na Baraza Kuu la Kiislamu Tanzania (BAKWATA) sherehe hizo zilifanyika VINGUNGUTI Wilayani Ilala juzi (Picha na Heri Shaban)

Na Heri Shaban
BARAZA kuu la Kiislamu Tanzania (BAKWATA) umetoa wito kwa watu wanaomiliki Mali za waislamu kwa njia isiyokuwa ya halali wajitokeze kurudisha.

Wito huo umetolewa Dar es salaam Leo na KATIBU wa BAKWATA Tanzania Nuhu Jabir,katika Salaam za Baraza    Kuu la Waislam Tanzania BAKWATA kwenye  baraza la Eid El haj viwanja vya VINGUNGUTI Wilaya ya Ilala.


Jabir alisema   katika kuzinusuru Mali za Waislam kutoka katika mikono ya Watu binafsi jitihada kibwa zinafanywa na zinaonyesha mwelekeo mzuri na tunawakikishia Waislam kwamba mali hizo zitarudi na kusimamiwa na waislam wenyewe.


"Tupo katika kipindi cha kujisahihisha kutokana na makosa yaliofanywa huko nyuma na baadhi ya viongozi wetu kulifanya baraza kuwa hoi kiuchumi ikiwemo kumilikisha Mali za waislamu za WAKFU kwa watu binafsi "alisema Jabir.


Jabir alisema BAKWATA inazidi kujipanga kuimalisha uchumi wake ili kuinua na kuufanya uwe endelevu  na kutambua dhahir kwamba dini hupiganiwa kwa Mali kabla ya nafsi.Baada ya imani ,ujenzi wa misingi imara ya uchumi na fedha katika jamii bora ya Kiislamu.

"BAKWATA kupitia Kauli mbiu yetu jitambue, Badirika ,na acha mazoea, tupo katika kipindi cha kujisahihisha kutokana na makosa yaliofanywa huko nyuma na baadhi ya viongozi wetu na kulifanya baraza kuwa hoi kiuchumi.

Alisema baraza hilo kwa sasa lipo katika hatua nzuri kujimalisha kiutendaji ili kuwatumikia waislamu wote nchini chini ya farsafa ya Jitambue, badirika, acha mazoea ni wakati muafaka kwa baraza kushika hatamu za uongozi wa waislam na dhima ya kwanza ya mabadiliko katika nafasi mbalimbali.

 Alisema wana ungana na Mufti wa Tanzania kuleta mabadiliko ya kweli katika ngazi mbalimbali za uongozi na utendaji na kuakikisha kila kiongozi anatekeleza majukumu yake na kuheshimu mipaka ya madaraka Kama ilivyoainishwa kikatiba.

Aidha alisema asiye tayari kuendana na falsafa hiyo ya mabadiliko ajiondoe kwa hiari vunginevyo kumbo la mabadiliko litamkumba pembeni.

Alisema hivi karibuni Waziri mkuu Kassim Majaliwa alifungua mkutano wa viongozi wa dini, CCT mjini Dodoma, alitoa wito kwa taasisi za dini kuungana na Serikali katika ujenzi wa viwanda Tanzania.

Jabir alisema  Kutokana na wito huo maridhawa WAZIRI MKUU kwa viongozi wa dini Tanzania, BAKWATA kwa sasa ipo katika utafiti wa Hali ya juu namna waislam kupitia Bakwata washiriki kwa dhati katika kuanzisha viwanda mbalimbali mikoani kwa kuzingatia sheria na taratibu za kuendesha viwanda.

Kwa upande Wake Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt, Hussein Mwinyi amewataka Waislam na Watanzania kwa ujumla kuendelea kudumisha amani.

Dkt. Mwinyi alisema Serikali ya awamu ya tano itaendelea kudumisha amani ya nchi  ,amewataka Waislamu nchini kudumisha ibada na Wale wenye uwezo kwenda hija Saudi Arabia Macca .

Aliwataka Waislam kudumisha MAENDELEO pamoja na kuunga mkono BAKWATA uwanzishwaji wa Viwanda.




Hivyo makala BAKWATA yawataka Wanaomiliki Mali za Waislam kwa njia isiyo ya halali kuzirudisha

yaani makala yote BAKWATA yawataka Wanaomiliki Mali za Waislam kwa njia isiyo ya halali kuzirudisha Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala BAKWATA yawataka Wanaomiliki Mali za Waislam kwa njia isiyo ya halali kuzirudisha mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/bakwata-yawataka-wanaomiliki-mali-za.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "BAKWATA yawataka Wanaomiliki Mali za Waislam kwa njia isiyo ya halali kuzirudisha"

Post a Comment