title : ADIWANI TABORA WAUNGA MKONO UJENZI WA UZIO KATIKA STENDI MPYA KUONGEZA MAPATO
kiungo : ADIWANI TABORA WAUNGA MKONO UJENZI WA UZIO KATIKA STENDI MPYA KUONGEZA MAPATO
ADIWANI TABORA WAUNGA MKONO UJENZI WA UZIO KATIKA STENDI MPYA KUONGEZA MAPATO
Mwamba wa habari
BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora limeunga mkono uamuzi wa Menejimenti ya Halmashauri hiyo wa kujenga uzito wa kuzunguka Stendi mpya ikiwa mni sehemu ya kuongeza chanzo cha mapato.
Akizungumza wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani leo mjini Tabora Diwani wa Kata ya Ndevelwa Selemani Maganga kwa niaba ya Madiwani alisema mpango huo ni mzuri na utasaidia kuongeza mapato kutokana na kiingilio cha wasindikizaji.
Alisema kimsingi wanaounga mkono jitihada hizo lakini ni vema gharama ya ujenzi zikapunguzwa kutoka milioni 54 kuwa chini ya hapo.
Maganga alisema ujenzi wa ukuta hauitajiki bali ni kuweka waya zitakazo lazimisha watu kutumia milango wakati wa kuingia na kutoka na kujenga banda la gharama nafuu kwa ajili ya wasafiri.
Alisema mipango ya baadae ya Halmashauri hiyo ni kuhamisha Stendi kutoka ilipo kwenda nje ya mji , hivyo ni vema kuweka fedha kidogo hapo wakati wakianza maandalizi ya kuhamisha Stendi ilipo hivi sasa.
Awali akitoa taarifa kuhusu mpango wa kukusanya mapato na kuendesha matangazo katika Stendi hiyo Afisa Ugavi wa Manispaa hiyo Mathias Lukala alisema walitangaza katika vyombo vya habari kwa jili ya kumpata wakala wa ukusanyaji mapato katika Stendi hiyo lakini walifanikiwa kumpata mwombaji mmoja.
Alisema baada ya kukaa naye kwa ajili ya makubaliano ya kiwango kwa kuiilipa Halmashauri hiyo alidai awe anawalipa shilingi 200,000/- kwa kipindi cha masika na 350,000/- kwa siku fedha ambayo waliona ni kidogo na ndipo walifikia uamuzi wa kukusanya wenyewe.
Lukala alisema kuanzia Septemba Mosi mwaka huu makusanyo yote ya Stendi hiyo mpya yatafanywa na Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.
Baada ya ufafanuzi huo Madiwani kwa kauli moja waliunga mkono hatua na uamuzi uliochukuliwa na Menejimenti ya Manispaa ya Tabora kuhusu ukusanyaji wa mapato katika Stendi hiyo.
Hivyo makala ADIWANI TABORA WAUNGA MKONO UJENZI WA UZIO KATIKA STENDI MPYA KUONGEZA MAPATO
yaani makala yote ADIWANI TABORA WAUNGA MKONO UJENZI WA UZIO KATIKA STENDI MPYA KUONGEZA MAPATO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ADIWANI TABORA WAUNGA MKONO UJENZI WA UZIO KATIKA STENDI MPYA KUONGEZA MAPATO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/adiwani-tabora-waunga-mkono-ujenzi-wa.html
0 Response to "ADIWANI TABORA WAUNGA MKONO UJENZI WA UZIO KATIKA STENDI MPYA KUONGEZA MAPATO"
Post a Comment