ZURA Yatangaza Bei Mpya ya Mafuta Zanzibar Kuazia leo 11/7/2018

ZURA Yatangaza Bei Mpya ya Mafuta Zanzibar Kuazia leo 11/7/2018 - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa ZURA Yatangaza Bei Mpya ya Mafuta Zanzibar Kuazia leo 11/7/2018, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : ZURA Yatangaza Bei Mpya ya Mafuta Zanzibar Kuazia leo 11/7/2018
kiungo : ZURA Yatangaza Bei Mpya ya Mafuta Zanzibar Kuazia leo 11/7/2018

soma pia


ZURA Yatangaza Bei Mpya ya Mafuta Zanzibar Kuazia leo 11/7/2018

Na Mwashungi Tahir,-  Maelezo     11-7-2016.
Mkuu wa Kitengo cha  uhusiano cha Mamlaka ya Udhibiti Huduma za Maji  na Nishati (ZURA) Khuzaimat Bakari Kheir  ametoa taarifa juu ya bei mpya za mafuta zitakazoanza kutumika rasmi kuanzia leo siku ya Jumatano ya tarehe 11-07-2018.
Hayo ameyasema leo huko katika ukumbi wao wa mkutano uliopo Maisara wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu ongezeko kwa  bei mpya za mafuta itakayoanza leo .
Alisema ZURA imepanga bei kwa kwa kuzingatia mambo yafuatayo ikiwemo wastani wa mwenendo wa mabadiliko wa bei za mafuta katika soko la dunia (Platts Quatations) katika mwezi wa Juni, 2018, kwa lengo la kupata kianzio cha kufanya mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi Julai 2018.
Pia alisema gharama za uingizaji na uhifadhi wa Mafuta katika Bandari ya Dar es salaam pamoja na gharama za kuyasafirisha tena hadi Zanzibar, gharama za usafiri , Bima na ‘Premium ‘ hadi Zanzibar.
Aidha alisema thamani ya shillingi ya Tanzania  kwa Dola , kodi za Serikali  na pia kiwango cha faida kwa wauzaji wa Jumla na Reja reja.
Amesema Bei za mafuta za Petrol , Dizeli, Mafuta ya Taa na Mafuta ya ndege (Jet-AL) zimepanda katika mwezi wa Julai , 2018 ikilinganishwa na bei za mwezi wa Juni 2018 kutokana na kupanda kwa wastani wa uuzaji wa bidhaa hizo katika soko la Dunia(Platts FOB) kwa mweziJuni 2018.
Vile vile alisema Bei ya Reja reja ya mafuta ya Petroli kwa mwezi wa Julai , 2018 imepanda kwa Tsh . 180 kwa lita kutoka Tsh . 2,255 ya Mwezi wa Juni, 2018 hadi Tsh 2, 435 kwa lita katika mwezi wa Julai. 2018 sawa na ongezeko la asilimia 8%.
Aliendelea kuelezea bei mpya ya mafuta ya Dizeli kwa mwezi wa Julai , 2018 imepanda kwa Tsh 180 kwa lita kutoka Tsh 2, 250  ya mwezi wa Juni 2018  hadi Tsh . 2,431 sawa na ongezeko la asilimia 8%.
Bei ya reja reja ya Mafuta ya Taa kwa Mwezi wa Julai . 2018 imepanda kwa Tsh . 37 kwa lita kutoka Tsh 1,740 ya mwezi wa Juni 2018 hadi Tsh.1,777 sawa na ongezeko la asilimia 6.9%.
Sambamba na hayo alieleza bei ya reja reja  ya Mafuta ya ya Meli (Banka) kwa mwezi wa Julai , 2018 imepanda  kwa Tsh. 167 kwa lita kutoka Tsh 2,092 katika Mwezi wa Juni , 2018 hadi Tsh 2,259 katika mwezi wa Julai , 2018  sawa na ongezeko la asilimia 8%.
Hata hivyo alisema Bei ya Reja reja ya mafuta ya Ndege kwa Mwezi wa Julai , 2018 imepanda kwa Tsh .126 kwa lita kutoka Tsh 1,884.51 kwa lita katika Mwezi wa Juni, 2018 hadi Tsh . 1,936.73 katika mwezi wa Julai , 2018 sawa na ongezeko la asilimia 6.9%.
Mwisho .


Imetolewa na Habari Maelezo.


Hivyo makala ZURA Yatangaza Bei Mpya ya Mafuta Zanzibar Kuazia leo 11/7/2018

yaani makala yote ZURA Yatangaza Bei Mpya ya Mafuta Zanzibar Kuazia leo 11/7/2018 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala ZURA Yatangaza Bei Mpya ya Mafuta Zanzibar Kuazia leo 11/7/2018 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/zura-yatangaza-bei-mpya-ya-mafuta.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "ZURA Yatangaza Bei Mpya ya Mafuta Zanzibar Kuazia leo 11/7/2018"

Post a Comment