title : WADAU MKOANI TABORA WAOMBWA KUSAIDIA UJENZI NYUMBA KWA AJILI YA MAKAZI YA POLISI
kiungo : WADAU MKOANI TABORA WAOMBWA KUSAIDIA UJENZI NYUMBA KWA AJILI YA MAKAZI YA POLISI
WADAU MKOANI TABORA WAOMBWA KUSAIDIA UJENZI NYUMBA KWA AJILI YA MAKAZI YA POLISI
NA TIGANYA VINCENT
KAMPUNI na wadau mbalimbali Mkoani Tabora wameomba kusaidia ujenzi wa nyumba kwa ajili ya Askari Polisi ambao wanakabiliwa na uhaba wa nyumba za kuishi na hivyo kulazimika kupanga uraini.
Ombi hilo limetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akipokea msaada wa mifuko 600 za Saruji zenye thamani ya milioni 10,800,000/- uliotolewa na Kampuni ya ununuzi wa Tumbaku ya Alliance One.
Alisema kuwa Askari wengi wa vyeo vya chini wanalazimika kupanga uraini jambo ambalo kwa kiasi kikubwa linapunguza ufanisi katika kupambana na uhalifu.
Mwanri alisema kwa mujibu taarifa za Askari Polisi inaonyesha kuwa Polisi wapatao 853 wanaishi uraiani na wanaoishi kambini ni 327 jambo ambalo sio zuri katika kuleta ufanisi wa utendaji wa Jeshi hilo.
Alisema mpaka hivi sasa jitihada za awali za kuandaa michoro ya ramani za nyumba ambazo zinatarajiwa kujengwa na hivyo kuwaomba wafanyabiashara, Kampuni kujitokeza kuchukua kwa ajili kuwajengea kwa kadiri watakavoweza.
“Tuko kwenye kampeni ya kuwajengea vijana wetu Polisi nyumba za kuishi …tunaomba safari hii badala ya kutuletea vifaa kama vile saruji, nondo , bati mtusaidie kujenga nyumba za askari Polisi na mutukabidhi vifunguo mkishamaliza kujenga …asakari wetu wengi hawana nyumba na hivyo kulazimika kuishi uraiani…tunawaomba Alliance One, Kampuni nyingine na wadau watakaoguswa na tatizo hilo la asakari wetu mutusaidie kwa hilo…makazi ya uhakika ya Polisi yatasaidia kuleta ufanisi “ alisisitiza.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa ufafanuzi jana kabla ya kupokea msaada wa mifuko 600 ya saruji yenye thamani ya shilingi 10.8 kutoka Kampuni ya Alliance One Tobacco Tanzania.
Mkurugenzi wa Uzalishaji wa ampuni ya Alliance One Tobacco Tanzania David Mayunga akitoa maelezo mafupi jana kabla ya kukabidhi msaada wa mifuko 600 ya Saruji kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora kwa ajili ya ujenzi wa Hosteli za watoto wa kike na Wodi ya Wakinamama.
Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Abel Busalama akitoa maelezo mafupi jana kabla ya kupokea msaada wa mifuko 600 ya Saruji kutoka Kampuni ya Alliance One Tobacco Tanzania.
Katibu Tawala Wilaya ya Tabora Sweetbert Nkuba akitoa maelezo mafupi jana kabla ya kupokea msaada wa mifuko 600 ya Saruji kutoka Kampuni ya Alliance One Tobacco Tanzania.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akishirikiana na viongozi mbalimbali kupokea msaada jana wa mifuko 600 ya Saruji kutoka Kampuni ya Alliance One Tobacco Tanzania.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WADAU MKOANI TABORA WAOMBWA KUSAIDIA UJENZI NYUMBA KWA AJILI YA MAKAZI YA POLISI
yaani makala yote WADAU MKOANI TABORA WAOMBWA KUSAIDIA UJENZI NYUMBA KWA AJILI YA MAKAZI YA POLISI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WADAU MKOANI TABORA WAOMBWA KUSAIDIA UJENZI NYUMBA KWA AJILI YA MAKAZI YA POLISI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/wadau-mkoani-tabora-waombwa-kusaidia.html
0 Response to "WADAU MKOANI TABORA WAOMBWA KUSAIDIA UJENZI NYUMBA KWA AJILI YA MAKAZI YA POLISI"
Post a Comment