title : ZFDA Yaangamiza Tani 95 za Chakula na Tani Moja ya Dawa za Binaadamu Zilizomaliza Muda wa Matumizi.
kiungo : ZFDA Yaangamiza Tani 95 za Chakula na Tani Moja ya Dawa za Binaadamu Zilizomaliza Muda wa Matumizi.
ZFDA Yaangamiza Tani 95 za Chakula na Tani Moja ya Dawa za Binaadamu Zilizomaliza Muda wa Matumizi.
SEHEMU ya bidhaa ya Mchele na Unga wa Ngano na Sembe zikiteremshwa katika magari kwa ajili ya Kuangamizwa katika Jaa la Kibele Wilaya ya Kati Unguja.
FUNDI wa mageti akikata geti la Ghala lililokua likihifadhiwa bidhaa za Mchele, Unga wa ngano na sembe uliomaliza muda na haufai kwa matimizi ya Binadamu katika mtaa wa Migombani Mjini Zanzibar.
SEHEMU ya bidhaa ya Mchele na Unga wa Ngano na Sembe zikiteremshwa katika magari kwa ajili ya Kuangamizwa katika Jaa la Kibele Wilaya ya Kati Unguja. GARI ya Kijiko likiuharibu kwa kuufukia Unga wa Ngano uliokua haufai kwa matumizi ya Binadamu katika Jaa la Kibele Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
DAWA za binadamu za aina mbali mbali za kuondosha maumivu na Virutubisho zilizo angamizwa katika Jaa la Kibele Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja
GARI la Kijiko likiangamiza Dawa za kuondosha maumivu na Virutubisho zilizoangamizwa katika Jaa la Kibele Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja
MKURUGENZI Idara ya Udhibiti na Usalama wa Vyakula wa ZFDA Dkt. Khamis Ali Omar akizungamza na Waandishi wa habari wakati wa zoezi la kuangamizaji Bidhaa zisizofa kwa Matumizi ya Binadamu lililofanyika katika Jaa la Kibele Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja. Picha na Abdalla Omar Maelezo - Zanzibar.
Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar 16.7.2018
Mamlaka ya Chakula na Dawa Zanzibar (ZFDA) imejidhatiti
kuhakikisha kuwa bidhaa zinazoingizwa nchini zinawafikia
wananchi zikiwa salama kwa matumizi kwa lengo la kulinda
afya zao.
Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti wa Usalama wa chakula wa
ZFDA Dkt. Khamis Ali Omar alieleza hayo katika jaa la
Kibele wakati wa kazi ya kuangamiza tani 95 za bidhaa za
mchele, sembe na Unga wa ngano pamoja na tani moja ya
dawa za binadamu.
Alisema bidhaa za chakula zilizoangamizwa za
mfanyabiashara Mohamed Mattar ziliharibika baada ya
kuhifadhiwa kwa muda mrefu katika maghala yasiyorasmi
na yaliyokosa sifa za kutumika kwa kazi hiyo.
Dkt. Khamis alieleza kuwa kutokana na maghala hayo
kukosa viwango vinavyokubalika na kutosajiliwa na ZFDA,
mfanyabiashara Mattar alikuwa akiweka bidhaa zake kwa
siri wakati wa usiku.
Akitaja viwango vya bidhaa zilizoangamizwa, Mkurugenzi wa
Idara ya Udhibiti na uhifadhi wa chakula wa ZFDA alisema
mchele ulikua tani 52, unga wa ngano tani 37 na sembe
ilikuwa tani sita.
Alisema sehemu ya bidhaa hizo zilikuwa zikitolewa kama
sadaka katika mwezi wa Ramadhani kama mbinu ya
mfanyabiashara huyo kujaribu kukwepa gharama za
kuangamiziwa bidhaa zake.
Mkurugenzi Idara ya Udhibiti na Usalama wa Chakula
aliwataka wafanyabiashara wanapotaka kutoa sada ya
chakula kuishirikisha ZFDA ili kuhakikisha ubora na usalama
wa bidhaa itakayotolewa.
Mfamasia wa ZFDA Nassir Buheti alisema kiwango kikubwa
cha dawa zilizomaliza muda wa matumizi zilitoka Taasisi za
kiraia (NGO) kwa ajili ya kuangamizwa na kiwango kidogo
kilipatikana katika maduka ya kuuzia dawa.
Buheti alitoa wito kwa maafisa wa NGO wanaopata msaada
wa dawa kutoka nje kuwa waangalifu katika kuzitumia na
inapokaribia miezi mitatu kabla ya kumaliza muda wa
matumizi na wakihisi haziwezi kumalizika wazipeleka ZFDA
ili wazisambaza katika vituo vya afya vya Serikali ambako
mahitaji ya dawa ni makubwa.
Hivyo makala ZFDA Yaangamiza Tani 95 za Chakula na Tani Moja ya Dawa za Binaadamu Zilizomaliza Muda wa Matumizi.
yaani makala yote ZFDA Yaangamiza Tani 95 za Chakula na Tani Moja ya Dawa za Binaadamu Zilizomaliza Muda wa Matumizi. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ZFDA Yaangamiza Tani 95 za Chakula na Tani Moja ya Dawa za Binaadamu Zilizomaliza Muda wa Matumizi. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/zfda-yaangamiza-tani-95-za-chakula-na.html
0 Response to "ZFDA Yaangamiza Tani 95 za Chakula na Tani Moja ya Dawa za Binaadamu Zilizomaliza Muda wa Matumizi."
Post a Comment